VPL 2015/2016:-Tambwe apiga hat-trick Yanga SC ikishinda 5 na kurudi Kileleni mwa Ligi Kuu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 21, 2016

VPL 2015/2016:-Tambwe apiga hat-trick Yanga SC ikishinda 5 na kurudi Kileleni mwa Ligi Kuu.

Yanga 3
Amis Tambwe ameibuka shujaa kwenye mchezo wa Yanga vs Majimaji baada ya kutupia kambani goli tatu (hat-trick) wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 5-0 na kupaa tena hadi kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.


Yanga 4
Ligi Kuu Vodacom, VPL, iliendelea Leo January 21,2016 kwa Mabingwa Watetezi Yanga SC kuitandika Majimaji FC bao  5 - 0  katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kurudi tena kwenye Kiti chao cha uongozi wa Ligi huku Straika wao Amisi Tambwe akipiga Hetitriki.

Yanga SC walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 4 kupitia Thaban Kamusoko na Bao hilo kudumu hadi Mapumziko.

Yanga 1
Bao la Pili la Yanga SC lilifungwa Dakika ya 47 na Donald Dombo Ngoma baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Thaban Kamusoko.

Katika Dakika ya 57 Amisi Tambwe aliipa Yanga SC Bao la 3 na hilo ni Bao lake la 11 kwenye VPL likimfanya azidi kupaa juu kileleni katika Safu ya Mfungaji Bora.

Yanga
Tambwe tena akaipa Yanga SC Bao la 4, likiwa Bao lake la 12 kwenye VPL, katika Dakika ya 72 baada ya muvu murua ya Timu ya Yanga SC .

Yanga SC walifunga Bao lao la 5 Dakika ya 88 Mfungaji akiwa tena Tambwe akipiga Bao hilo, likiwa lake la 13 kwa VPL, na ni Hetitriki kwa Mechi hii.

Ushindi huu umewapa Yanga SC uongozi wa VPL wakiwa na Pointi 39 kwa Mechi 15 sawa na Azam FC lakini wao wako juu kwa ubora wa Magoli.

Matokeo ya mechi nyingine zilizopigwa leo kwenye viwanja tofauti na uwanja wa taifa ni kama ifuatavyo:

Mwadui FC 2-1 Kagera Sugar

Mtibwa Sugar 0-0 African Sports

Yanga 2
LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA 2015/2016.

Ratiba:

Jumamosi Januari 22,2016.

Coastal Union v Yanga SC

Simba SC v African Sports

JKT Ruvu v Majimaji

Tanzania Prisons v Azam FC

Mtibwa Sugar v Stand United

Mwadui FC v Toto Africans

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad