Waziri wa
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako
amefuta mfumo wa matokeo ya GPA kwa wanafunzi wa kidato cha nne, sita na ualimu
na kurudisha ule wa zamani wa divisheni.
Mbali na
hilo, Ndalichako ameagiza kuondolewa kwa mtihani wa pili (paper two) kwa
watahiniwa binafsi ambao ulianza mwaka 2014.
Katika
mkutano na waandishi wa habari jana,January 20,2016, Profesa Ndalichako alisema Serikali
haitawavumilia watu ambao wanataka kuchezea elimu.
“Nilitembelea
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Januari 7, nikaagiza wanipe sababu za
msingi za kutoka divisheni kuingia GPA, hadi leo wameleta maelezo bila ya
sababu za msingi na maelezo yao yamejikita katika blabla ambazo
hazijitoshelezi,” alisema Profesa Ndalichako ambaye katika mkutano huo aliongozana
na naibu wake, Stella Manyanya na Katibu Mkuu wa Necta, Dk Charles Msonde.
Alisema kuna
mgongano mkubwa katika upangaji wa GPA kwani kidato cha nne ufaulu unaanzia 3.6
-5, kidato cha sita katika daraja hilo wanaanzia 3.7 -5 wakati ufaulu kama huo kwa
mafunzo ya ualimu unaanzia 4.4 -5 ambao ni mkanganyiko mkubwa unaozalisha watu
wasio na ubora wa kiwango husika.
“Baadhi ya
watahiniwa waliopitia katika mfumo huo na kufaulu wanaonyesha kiwango kidogo
cha maarifa kuliko kiwango cha ufaulu,” alisema.
Alisema
kuwapo gredi E kwenye alama za ufaulu wakati haihesabiki katika upangaji wa
GPA, kunawafanya watahiniwa waliopata E kujiona wako bora kuliko wenye D mbili
na F zote ambao wanahesabiwa wamefaulu.
Alisema
Necta imetoa maelezo mengi ambayo yameonekana hayana uhalisia wala wa
kukamilisha sababu badala yake wamejikita katika visingizio.
Alisema
Necta walimweleza kuingia katika mfumo huo ilikuwa ni maoni ya wadau lakini
alipowauliza ni wadau kiasi gani na mikutano hiyo ilifanyikia wapi, hawakuwa na
majibu na hakuna hata mkutano ambao uliwahi kufanyika.
“Jambo
jingine lazima mkumbuke kuwa, mfumo huu haujaenda hata kwa kamishna wa elimu
kupata kibali, ndiyo maana wadau waliniambia kuwa nisingetoa siku saba badala
yake ningeufuta mara moja,” alisema Ndalichako.
Alipinga
madai kwamba uliruhusiwa na Serikali, akisema ulianza kutumika tangu 2014
wakati maagizo ya Serikali Mtandao (EG) yalieleza kuwa kila kitu kianze
kutumika Juni 16, mwaka huu.
Alisema
alidanganywa kwa kuambiwa wizara iliagiza wakati amebaini kuwa wizara
ilipitisha kanuni za mitihani Oktoba 28, 2015 na kuingiza katika gazeti la
Serikali Novemba 6 mwaka jana ikiwa ni miaka miwili tangu mfumo wa GPA uanze
kutumika.
Kwa upande
wa watahiniwa binafsi, alisema kuanzia sasa hakutakuwa na mitihani miwili
ambayo mmoja ulikuwa ni kwa ajili ya upimaji endelevu, hivyo watahiniwa
watafanya mtihani mmoja tu.
Hata hivyo,
Dk Msonde alisema watahiniwa binafsi wa sasa watasahihishiwa mitihani yao kwa
mfumo wa mitihani miwili kwa kuwa walishafanya.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii,
Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha
kwa WhatsApp +255789925630 .
|
No comments:
Post a Comment