UHURU DAY DECEMBER 09:-Rais Magufuli Awaongoza Watanzania Kufanya Usafi . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, December 09, 2015

UHURU DAY DECEMBER 09:-Rais Magufuli Awaongoza Watanzania Kufanya Usafi .

 Rais wa Tanzania,Dr John Magufuli kiungana na wananchi katika kufanya usafi leo December 09,2015 ikiwa ni UHURU DAY na pichani akiwa katika eneo la Feri jijini Dar es Salaam, akiwa amekaa ndani ya kifaa duni cha kufanyia uvuvi maarufu kama ‘mtumbwi’ usio na mashine.

Rais wa Tanzania,Dr .John Magufuli leo ameongoza kwa vitendo zoezi la kufanya usafi , kama alivyoelekeza baada ya kufuta shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika leo, Disemba 9.

Rais Magufuli na mkewe Janeth wamefanya usafi katika maeneo ya Feri, eneo ambalo liko mita kadhaa kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya zoezi hilo, Dk. Magufuli aliwashukuru watanzania wote kwa ujumla kwa kuitikia wito wake wa kufanya usafi huku akieleza kuwa hili linapaswa kuwa zoezi endelevu kwani uchafu hauwezi kuisha kwa kufanya usafi mara moja kwa mwaka.
Wananchi kwa ujumla nchini wameonekana kuitikia wito wa kufanya usafi katika maeneo yao kwa hamasa kubwa hali inayoonesha kuwa Tanzania itaweza kutokomeza magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uchafu.

 Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

Post Bottom Ad