TAZAMA PICHA:-DC Ngara azindua Kampeni ya ABIRIA PAZA SAUTI na kuwahimiza Abiria kutambua haki na wajibu wao wawapo safarini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, December 09, 2015

TAZAMA PICHA:-DC Ngara azindua Kampeni ya ABIRIA PAZA SAUTI na kuwahimiza Abiria kutambua haki na wajibu wao wawapo safarini.

Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bi Honoratha Chitanda (pichani) akigawa vipeperushi vyenye elimu kwa Abiria, wakati akizindua Kampeni ya ABIRIA PAZA SAUTI kwa Abiria na Madereva,wilayani Ngara December 08,2015, Kampeni  inayoendeshwa na taasisi ya mabalozi wa Usalama barabarani, yaani Road Safety Ambassadors (RSA) Tanzania kwa ajili ya kukuza uelewa na kuwahimiza watanzania kutambua haki na wajibu wao wawapo safarini kama abiria.

Abiria wanaosafiri kati ya Ngara,Kahamaakisoma Kipeperushi chenye elimu kuhusu abiria na haki zake awapo safarini wakati akizindua Kampeni ya ABIRIA PAZA SAUTI kwa Abiria na Madereva,wilayani Ngara,mkoani Kagera December 08,2015.

Akizindua Kampeni hiyo, Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bi Honoratha Chitanda ,amesema:- jukumu la kuzuia ajali halipaswi kuachwa kwa Jeshi la Polisi pekee bali hata Madereva na abiria wana wajibu huo kwa kuzingatia sheria na alama za Barabarani huku abiria wakitakiwa kutoa taarifa za ukiukwaji wa sheria unaofanywa na Dereva kwenye mamlaka husika ili hatua zichukuliwe.


Pichani ni Mratibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani, RSA Kanda ya Ziwa Magharibi Bw Abel Ntahorutaba akitoa hatuba fupi wakati wa uzinduzi huo na kubainisha kuwa, ajali nyingi hutokea kutokana na uzembe wa Madereva, kubeba abiria kuliko uwezo wa vyombo vyao sambamba na mwendo kasi na hivyo kusababisha vifo na ulemavu.

 Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

Post Bottom Ad