UEFA LEAGUE 2015/2016:-Matokeo kamili ya mechi za UEFA zilizochezwa Jumatano December 09,2015 na Timu 16 zilizofuzu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 10, 2015

UEFA LEAGUE 2015/2016:-Matokeo kamili ya mechi za UEFA zilizochezwa Jumatano December 09,2015 na Timu 16 zilizofuzu.

Olivier Giroud alifungia Arsenal mabao matatu kwa mara yake ya kwanza na kuhakikisha Arsenal  wanaendeleza rekodi yao nzuri Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kufika hatua ya 16 bora kwa kuichapa  Olympiakos.

Arsenal walihitaji kushinda kwa mabao mawili wazi lakini walipata mabao hata zaidi na kumaliza wa pili Kundi F.

Giroud alianza kwa kufunga kwa kichwa kipindi cha kwanza, kisha akafunga la pili kipindi cha pili kwa usaidizi kutoka kwa Joel Campbell.

Mfaransa huyo alihakikisha Arsenal wanafuzu kwa kufunga la tatu kupitia penalti.
 
Arsenal hawajawahi kukosa kufika hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tangu kuanza kwa mfumo wa sasa 2003-4, na walionyesha uzofu wa kusakata gozi katika jukwaa kuu Ulaya kwa kung’aa Athens.
Takwimu muhimu:
  • Olivier Giroud ndiye mchezaji wa nne kufungia Arsenal hat-trick kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (baada ya Thierry Henry, Nicklas Bendtner na Danny Welbeck).
 
  • Vijana wa Arsene Wenger wameshinda mechi yao ya kwanza Ugiriki tangu Desemba 1998 (3-1 dhidi ya Panathinaikos).
 
  • Giroud ndiye mchezaji was aba wa Arsenal kufikisha magoli kumi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (wengine wakiwa Henry, van Persie, Ljungberg, Fabregas, Walcott na Pires the others).
 
  • Matokeo ya Jumatano yalifikisha kikomo msururu wa kutoshindwa wa Olympiakos wa mechi sita katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya timu za Uingereza(Kushinda 5, Sare 1)
 
  • Arsenal walikuwa wameshindwa mechi tatu zao za awali ugenini dhidi ya Olympiakos zote katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, zote katika mechi ya sita hatua ya makundi.


Chelsea nayo imekuwa timu ya tatu ya Uingereza kwenda 16 Bora ya michuano hiyo baada ya Manchester City na Arsenal, kufuatia ushindi wa mabao 2-0  dhidi ya FC Porto Uwanja wa Stamford Bridge katika mchezo wa Kundi G.

Ivan Marcano Sierra alijifunga dakika ya 12 kuipatia The Blues bao la kwanza kabla ya Willian Borges Da Silva kufunga la pili dakika ya 52.


Timu ambazo zimefanikiwa kutika hatua ya 16 ni pamoja na;- Real Madrid, PSG, VfL Wolfsburg, PSV Eindhoven, Atletico Madrid, Benfica, Man City, Juventus, FC Barcelona, Roma, FC Bayern Munich, Arsenal, Chelsea, Dynamo Kiev, Zenit St P na KAA Gent. Hapa chini ,Ni matokeo ya mechi zote zilizochezwa usiku wa December 09,2015 kuhitimisha hatua ya makundi kabla ya kuanza kwa hatua ya mtoano.
 Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

Post Bottom Ad