TAZAMA PICHA:-Namna Waziri Mkuu mstaafu alivyokabidhi ofisi kwa Waziri mkuu mpya Majaliwa Kassim.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, December 01, 2015

TAZAMA PICHA:-Namna Waziri Mkuu mstaafu alivyokabidhi ofisi kwa Waziri mkuu mpya Majaliwa Kassim..

Tayari uongozi mpya wa Serikali ya awamu ya tano,Nchini Tanzania, chini ya Rais Dk. John Magufuli umeanza kazi..ikiwa ni siku chache baada ya uteuzi wa Waziri mkuu Majaliwa Kassim kupewa madaraka, yapo mambo mengi ambayo tayari ameanza kuyatekeleza.

Jana ,November 30,2015, jioni kwenye ofisi ya waziri mkuu kulikuwa na hafla fupi ya makabidhiano kati ya waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda ambaye alimtembelea Waziri  mkuu mpya ikiwa ni pamoja na kumkabidhi ofisi.

Hapa chini tazama ni baadhi ya picha wakati wa makabidhiano hayo..

maja1
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkaribisha  Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda  ambaye Novemba 30,2015 alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kukabidhi Ofisi.
maja2
Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo  Pinda ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015 kukabidhi Ofisi.

maja3
Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda wakimsikiliza  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florence Turuka aliposoma taarifa kabla ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi Ofisi, kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015.

maja4
 
maja5
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa  akipokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutoka kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuujijini Dar es salaam Novemba 30, 2015.

maja6

maja7

maja8
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akifurahia  katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo  Pinda  na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florence Turuka baada ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi rasmi Ofisi ya Waziri  kwa  Waziri  Mkuu Majliwa , kwenye ukumbi wa Ofisiya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad