HAKUNA KUTUPA KITU:-… zile chupa unaziona takataka, Nigeria wamejengea mpaka nyumba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, November 30, 2015

HAKUNA KUTUPA KITU:-… zile chupa unaziona takataka, Nigeria wamejengea mpaka nyumba.

House3
Maisha yanabadilika kila siku, zamani ilikuwa ukikutana na chupa au makopo ya maji au juice unayaona takataka… sasahivi ni dili na watu wameweka nguvu zao kabisa kukusanya makopo na kuyauza !!

Nigeria wamefanya kitu kingine zaidi mtu wangu, umewahi kuona nyumba za makopo??!! Nigeria wamefanya kitu hicho, wamejenga nyumba kwa makopo ambapo ndani ya makopo hayo kumejazwa mchanga halafu makopo yanapangwa vizuri kabisa mpaka inakuwa nyumba ya kuishi.HABARI KWA HISANI YA MILLARDAYO.COM

Naija
Sifa nyingine kubwa za hizi nyumba ni kwamba zina uwezo wa kuzuia risasi na pia zinaweza kuzuia moto.Hapa Kazi ya ujenzi inaendelea namna hii, hatua kwa hatua!!
House7
Unaweza kuwa na swali kwamba chupa kiasi gani au chupa ngapi zinatosha kukamilisha mjengo??!! Jibu lake ni hili hapa, kama unahitaji nyumba ya vyumba viwili inatakiwa kuwepo na chupa 14,000… Umevutiwa na ujenzi wa aina hii mtu wangu ???
House4 House6 House8
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad