TAZAMA PICHA:-Mkutano wa 10 wa nchi za SADC Kuhamia Digitali Ulivyohitimishwa Dar - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 04, 2015

TAZAMA PICHA:-Mkutano wa 10 wa nchi za SADC Kuhamia Digitali Ulivyohitimishwa Dar



Picha na 4
Washiriki wa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Dar es salaam.

Picha na 1 Picha na 2
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene akifunga Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo jana,Desember 03,2015.

 Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo baada ya kuonekana kufanya vizuri katika uhamaji wa matumizi ya mfumo wa analogia kwenda digitali kwa wakati.

Picha na 3
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene (katikati) akiwaonesha jambo kupitia Kitumi chake cha Mkononi (IPAD) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Simba (kulia) na Naibu Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Bw. Fredrick Ntobi (kushoto) kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam.

Picha na 5
Mada mbalimbali zikiwasilishwa kwa washiriki wakati wa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam.

Picha Aron Msigwa – MAELEZO.Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad