KUKUA TEKNOLOJIA:-Mabasi yanayojiendesha yenyewe ( EZ 10 ) kutoa huduma Marekani. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 04, 2015

KUKUA TEKNOLOJIA:-Mabasi yanayojiendesha yenyewe ( EZ 10 ) kutoa huduma Marekani.

61

Muonekano wa basi hilo dogo aina ya EZ10 likiwa barabarani.
3052100-inline-s-3-robot-buses-are-coming-to-a-san-francisco-suburb

….Yakiwa yamepaki.
easymile_0012

ligier-easymile-ez10

 Abiria wakiwa ndani ya basi hilo.

Mabasi yenye kujiendesha yenyewe, yataanza kutumika nchini Marekani
hivi karibuni. 

Eneo la biashara la Bishop Ranch huko San Ramon, katika
jimbo la California, litakuwa sehemu ya kwanza nchini humo kutumia
mabasi yanayojiendesha yenyewe kwa mitambo maalum (robot) kusafirisha
abiria.

Hatua hiyo itakuwa ni mwanzo wa utaalam wa kuendeleza magari
yasiyokuwa na madereva kama yale yaliyoasisiwa na kampuni la Google
ambapo mtihani mkubwa utakuwa ni kwa watu kuyazoea magari hayo.


Hii inatokana na ukweli kwamba njia za sasa na kasi ya chini ya
maagari, havifanyizi mazingira mema kwa kuanzishwa kwa magari yasiyokuwa
na madereva.
 
EZ10 ni basi lisilokuwa na dereva ambalo ni maalum kwa safari fupi.
Gari hilo hivi sasa linafanya kazi barani Ulaya katika nchi za Finland
na Ufaransa na hivi karibuni litaanza kazi nchini Hispania.


Magari hnayo ambayo hutumia umeme, hubeba abiria wanaofikia kumi na
yana sehemu za kuwekea vigari vya kusukumwa vya walemavu (wheelchairs)
na waenda kwa miguu ambao wanaweza wakapanda.


Magari hayo yamelenga kumfanya abiria ‘kuyadandia’ na kukufikisha
mahali ambapo unakaribiakufika, na yamelengwa kwa kutumiwa katika sehemu
za bustani za mapumziko.


Magari hayo ya EZ10 hutumia njia zilizopangwa na kuendeshwa kwa
kutumia mitambo ya ‘laser’ ili kukwepa vitu vyovyote vilivyo katika njia
yanayopita. 

Njia hii ni nyepesi zaidi kuliko ile inayotumiwa na magari
ya Google ambayo ni lazima yakwepe au kupishana na magari mengine,
waenda kwa miguu na vikwazo vyovyote vinavyoweza kujitokeza wakati
yanapita kwa kasi katika barabara kuu.


Randell Iwasaki ambaye ni mkurugenzi wa kampuni la CCTA ambalo
hufanya majaribio ya magari yasiyokuwa na madereva liitwalo GoMentum
Station, anasema utaalam huu utawasaidia abiria kufika katika vituo vya
kusafiria, maeneo ya biashara na kwenye sehemu mbalimbali za huduma na
hivyo kukwepa adha ya kuendesha magari na kutafuta sehemu ya maegesho.BOFYA HAPA KUTAZAMA VIDEO YAKE JINSI YANAVYOFANYA KAZI.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad