MRATIBU UN:-Aridhishwa na Matumizi ya Ufadhiri Tabora. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 04, 2015

MRATIBU UN:-Aridhishwa na Matumizi ya Ufadhiri Tabora.


IMG_5447
Ofisa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas (kushoto) akisoma taarifa ya maendeleo ya miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mkoa wa Tabora. Pichani wa pili kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (wa tatu kushoto) wakipitia taarifa hiyo kwa pamoja kabla ya kuelekea kukagua miradi hiyo.

Na Modewji blog team, Tabora

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Mipango ya Maendeleo la Umoja huo Bw.Alvaro Rodriguez, amesema kwamba umoja huo utaendelea kufadhili miradi ya maendeleo katika mkoa wa Tabora yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi.

Hayo alisema jana baada ya kuzuru miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Tabora.

Miradi hiyo ni ya ujenzi wa bwawa la nguvumoja kwamtindo wa utoaji wa chakula kwa kazi inayofanywa na mradi wa misitu ya miyombo.

Katika ziara hiyo ambayo alikuwa na Ofisa kutoka Kitengo cha ushirikiano wa kimataifa wizara ya mambo ya nchi za nje, Bi. Maulidah Hassan Mratibu huyo aliridhishwa na mafanikio ya miradi hiyo ambayo imelenga kupiga vita umaskini na kutunza mazingira.

Ziara ya Mratibu huyo mkoani Tabora ni  moja ya ziara yake ndefu ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma.

Alipotoka Singida jana asubuhi alifika katika moja ya Wilaya kame nchini, Wilaya ya Igunga na kuona mradi unaofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) wa ukarabati wa bwawa la Charco.

Bwawa hilo ambalo litahudumia watu takribani 6,100 kutoka vijiji vya Nguvumoja, Ndembezi na Iborogelo lilijengwa awali na miradi ya TASAF lakini wakati wa mvua za Elnino tuta lake lilivurugika vibaya.

Akizungumzia bwawa hilokaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga ambaye pia ni Ofisa Kilimo na Ushirika wa Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas,  akizungumza alisema kwenye bwawa hilo kwamba Umoja wa Mataifa kupitia WFP wanawezesha ukarabati wa bwawa hilo kwa kutoa chakula kwa wachimbaji.

IMG_5482
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) aliyeambatana na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (wa pili kushoto) walipowasili kukagua mradi wa ujenzi wa Bwawa la Charco la Nguvumoja kwa mtindo wa utoaji wa chakula kutoka  Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwa kazi inayofanywa na mradi wa misitu ya Miyombo. Kushoto ni Ofisa Tawala msaidizi anayeshughulikia Uchumi na Tija wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Dkt. Phillips Mtiba pamoja na Ofisa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas (wa pili kulia).

Aidha imeelezwa kuwa tuta hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia kaya 1,200 na Ng’ombe elfu moja na kuweza kuhifadhi maji kwa mwaka mzima.

Imeelezwa kuwa wajenzi wanapewa debe moja la Mahindi kwa kina cha mita moja  na urefu wa mita nne na upana wa mita tatu na nusu lita ya mafuta ya kula na Njegere kilo tatu.

Kumalizika kwa bwawa hilo kutasaidia kupunguza umbali wa wananchi katika kutafuta maji.

Awali wananchi walilazimika kusafiri kilomita 30 kupata maji katika bwawa la Manzugi kuchota maji na kunywesha mifugo.

Aidha imeelezwa kuwa baadae wanyama watatengewa eneo la kunywa maji.

Aidha alitembelea kikundi cha ufugaji nyuki, utunzaji wa mazingira pamoja na usindikaji wa matunda pori cha Membo , wilayani Uyui.

Kikundi hicho kilichopo wilayani Uyui kimeanzishwa Mei 8,2007 na Katibu wa kikundi Nasibu Baraka alisema kikundi hicho chenye wanachama 30 kimefanyakazi kubwa ya kupiga vita umaskini.

Alisema ili kukabiliana na adui njaa na umaskini kikundi hicho kwa ufadhili wa UNDP kimewezesha kujiajiri wenyewe, Kusindika matunda ya asili kwa ajili ya jamu na divai,kilimo cha bustani, kilimo cha chakula na biashara, ujenzi wa majikobanifu,usagaji wa unga na kupika keki za Muhogo mbichi kwa Karanga na Asali.

Akisoma risala kwa Mratibu wa UN Tanzania alisema kwamba wamekuwa na mafanikio makubwa kutokana na ruzuku mbalimbali za UNDP ikiwamo mafunzo.

IMG_5486
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea kupata maelezo ya mradi huo.

Aidha amesema kwamba kwa sasa wanatumia sola badala ya mafuta ya taa huku mradi wa Miyombo ukiendelea kuleta neema.

Aidha ametaka umoja huo kuwasaidia kuwa na mshine za kisasa cha kusindika matunda na chakula.

Viongozi hao walifika katika mradi huo kuangalia mafanikio ya mradi huo unaotekelezwa chini ya mpango wa miaka mitano wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa,(UNDAP).

Aidha mradi huo umelenga kupunguza umaskini kutunza mazingira kwa njia ya uragibishi na na kufunza wananchi kuhusu suala la ufugaji nyuki na utunzaji wa mazingira.

Naye  Ofisa utawala msaidizi wa mkoa anayeshughulikia Uchumi na Tija Dk. Phillips Mtiba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Tabora, Ludovick Mwananzila ambaye hakuwepo kutokana na majukumu mengine kwenye  mikutano na wananchi kuhusu miradi ya TASAF, alisema baada ya kumaliza kukagua miradi kwamba wameridhika na miradi inayofadhiliwa na UN katika mkoa huo.

Alisema pamoja na kwamba walitembelea miradi michache lakini ni dhahiri mkoa wa Tabora umefurahishwa na misaada iliyotolewa ambayo inatia moyo na kusaidia harakati za serikali za kukomboa wananchi wake kutoka katika lindi la umaskini na ukosefu wa huduma muhimu kama za maji na hifadhi ya mazingira.

Pamoja na kushukuru kwa misaada hiyo kwa wanatabora na maendeleo yao, alitaka UN isiwachoke kusaidia vipaumbele vya mkoa huo ambavyo ni kujitokeza kwa chakula na hifadhi ya misitu.

IMG_5494
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na ukaguzi wa Bwawa hilo.

“ Nashukuru sana kwa msaada  tunaoendelea kupata kutoka UN kwa ajili ya maendeleo ya wana Tabora na Tabora kwa ujumla na niseme tu kwamba kama wana Tabora kuna vitu ambavyo tunaweza kufanya na mengine hatuwezi kuyafanya na hapo ndipo sasa tunapoweza kuona umuhimu wa nafasi ya wafadhili na wadau mbalimbali katika shughuli za maendeleo.” Alisema Dk. Phillips.

Alisema ingawa walikuwa na muda mfupi na kutembelea miradi michache , alitamani waje kurudi kuona miradi mingi zaidi ili watambue kwamba miradi hiyo inabadilisha wana Tabora na hawachezei fedha za ufadhili.

IMG_5496
Muonekano wa mradi wa ujenzi wa Bwawa la Charco la Nguvumoja.

Alisema suala la uhakika wa chakula kwa wananchi ni muhimu kwao kutokana na ukweli kuwa wananchi wakiwa na chakula hata fedha zao zitakaa mfukoni na kufanya kazi nyingine za maendeleo. Alisema kutokana na hali hiyo wataendelea kuomba kusaidiwa katika eneo hilo.

Aidha alitaka mkoa wa Tabora kuendelea kusaidiwa kutunza misitu ya Miyombo kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa misitu ni kivuta mvua na maji ndio pembejeo namba moja katika uzalishaji wa chakula.

Alishukuru UNDP kwa kusaidia kuhifadhi misitu hiyo ili kuwapo na uvunaji endelevu kwa kusaidia jamii kuitunza na kuismamia rasilimali hiyo na kuitumia katika fursa za kiuchumi kama ufugaji nyuki.

Leo Mratibu huyo ataendelea na ziara yake katika mkoa wa Kigoma.

IMG_5520
Wananchi wakiendelea kuchimba bwawa hilo.

IMG_5532
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nguvumoja watakaonufaika na mradi wa bwawa hilo.

IMG_5538
#HapaKaziTu; ndio maneno aliyokuwa akiyasema Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akichimbia sehemu ya bwawa hilo alipofanya ziara ya kukagua mradi huo wa Bwawa la Charco la Nguvumoja.

IMG_5540
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akichimba udongo na sururu huku Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akijaza udongo unaochimbwa kwenye ndoo.

IMG_5544
Mratibu Mkazi wa UN nchini Bw. Rodriguez akimwaga udongo aliokuwa akichimba katika bwawa hilo ikiwa ni ishara ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wanachi wa kijiji cha Nguvumoja katika Halmashauri ya Igunga.

IMG_5553
#HapaKaziTu; Wanakijiji pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakishangilia kwa pamoja huku wakiunga kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya #HapaKaziTu sambamba na mabango 17 ya malengo ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals-SDGs) walioyowafikia wanakijiji wa Nguvumoja. Kwa matukio zaidi bofya link hii

IMG_5583

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad