AJALI YA BASI LA TAKBIR:-Jeshi la Polisi limemkamata dereva aliye sababisha ajali na kuuwa watu 12 Iramba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 03, 2015

AJALI YA BASI LA TAKBIR:-Jeshi la Polisi limemkamata dereva aliye sababisha ajali na kuuwa watu 12 Iramba.


Basi la Takbir likiwa limeovaspeed kama kamera inavyoonesha na liliadhibiwa na Askari usalama barbarani kwa kupata notification  jana Desember 01,2015,jioni kabla ya ajali.

Jeshi la Polisi mkoani Singida limefanikiwa kumkamata dereva aliyesababisha ajali ya basi la Takbiri lililokuwa likitoka Dar-es-Salaam na kuelekea Geita kugongana na maroli mawili na kusababisha vifo vya watu kumina mbili katika barabara kuu ya Singida Mwanza ambayo imetokea katika kijiji cha Kizonzo wilayani Iramba.

Akiongea kwa njia ya simu akiwa katika eneo la ajali kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Singida ACP Thobias Sedoyeka amesema dereva huyo aliyetambulika kwa jina la Charles Kapema ambaye amekiri kosa kwa kusababisha ajali kwa uzembe amekamatwa wilayani Igunga na kusema kuwa aliamua kukimbia kwa kuhofia usalama wake.

Akiongea kwa shida huku akiwa amelazwa, Bi.Roda Mbata ambaye maarufu kwa jina la mama mchungaji Preje ni mmoja wa majeruhi pamoja na kusema dereva alikuwa akiendesha basi kwa mwendo wa kasi, ameliomba jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kushirikiana na serekali kupiga marufuku mabasi kusafiri usiku kwani madereva wengi wametumia mwanya huo kukimbiaza mabasi pindi askari wa usalama barabarani wanapo kuwa hawapo.

Katika hatua nyingine Kamanda Sedo Yeka amejibu swali la abiria aliyeomba mabasi ifikapo saa kumina mbili kusitisha safari na kulala, amekiri kuwa madereva wa mabasi wengi inapofika saa kumina mbili wakati askari hawapo huwa wana kimbiza sana mabasi, kwahiyo atahakikisha ombi hilo analifikisha katika ngazi husika ili lifanyiwe kazi.
  
Ajali hiyo ambayo imetokea ,Desember 01,2015, majira ya saa tatu usiku katika kijiji cha Kizonzo mpakani na wilaya ya Igunga na wilaya ya Iramba, dereva wa basi hilo awali alitozwa faini mkoani Singida kwa kuendesha basi kwa mwendo wa kasi, lakini adhabu hiyo haikuwa fundisho badala yake aliendelea na mwendo kasi na kusababisha ajali, vifoo na majeruhi bila sababu yoyote.Habari kwa Hisani ya ITV.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad