![]() |
|
Ndugu Halidi Abdu toka kijiji cha Shenda
chenye wakazi wapatao 2,800 katika kata ya Masumbwi wilaya ya Mbogwe mkoani
Geita;akihojiwa na mtangazaji wa redio free africa william bundala almaarufu
Kijukuu cha Bibi k akielezea jinsi walivyoweza kuwaadaa viongozi wao waweze
kuwasomea taarifa yao ya mapato na matumizi.Na Krantz Mwantepele, Geita
Ni miaka
mitatu na miezi nane toka mraghbishi Fedson Yaida na wenzake toka vijiji vya
jirani kukutana na Chukua Hatua. Ni rafiki waliyekutana naye mwaka 2011 katika
mazungumzo maalumu ambayo walitakiwa kuyafikisha kwa wananchi wenzao wa vijiji
vya Shenda, Iponya, Nyakasumula na Bukandwe katika wilaya ya Mbogwe mkoani
Geita.
Ni katika mazungumzo hayo ya siku tatu, ambayo Fedson toka kijiji cha
Shenda alibadilishwa na kuwa mraghbishi wa aling’amua uwezo alio nao katika
kusimamia rasilimali za kijiji chao, suala ni angezisimamiaje wakati yeye
si kiongozi na ni jukumu la wanakijiji
wote.
Katika mazungumzo hayo rafiki yao, Chukua Hatua aliwaambia, “Ni jukumu
lako Fedson na waraghbishi wengine mliopo hapa, ni jukumu lenu la msingi kuj i
t aj i r i sha kwa taarifa na maarifa. Kwa kufanya hivyo mtakuwa na uwezo wa
kujenga hoja mkizithibithisha na vielelezo.
Hivyo ni jukumu lenu kujua ni wapi
na toka kwa nani mtapata taarifa na vielelezo vya hoja yenu. Uzito wa hoja na
maelezo kwa uthibitisho ni silaha muhimu kama mnataka kushawishi wenz e n
u k u c h u k u a hatua.”
Baada ya maelezo hayo walitakiwa kwenda
kutembelea halmashauri ya wilaya yao, wakati huo ikiitwa Bukombe. Na baadhi ya
maeneo hayo ni ofisi za Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri.
Maelezo
haya yalilenga katika haki ya kupata taarifa, kwa mujibu wa ibara ya 18 ya
Katiba.
“Kweli
mazungumzo hayo yalinijengea uwezo mkubwa sana, Chukua Hatua alinipatia muongozo
na akanipangia kwenda kwa mkuu wa wilaya. Moja kwa moja nikaonana na DC
nikaanza kumuhoji mambo mbalimbali kuhusu pembejeo.
Ingawa majibu aliyonipa
sikuridhika nayo, lakini nilishukuru kupata nafasi ya kuongea naye. Na kwa
kweli tokea siku hiyo nikawa na ujasiri mkubwa sana,” Fedson Yaida akitoa
ushuhuda wa siku ambayo uoga ulimtoka.
Ujasiri huo
wenye msukumo wa ndani toka kwa mraghbishi mmoja kwenda kwa wenzake kwa njia ya
kuwashirikisha aliyopatiwa na Chukua Hatua, ndio umekuwa chanzo kikubwa cha mafanikio
ya pamoja ya wana Shenda katika kusimamia rasilimali zao.
Safari ya mwandishi
katika kijiji cha Shenda ilimtia moyo sana. Alikutana na waraghbishi toka
vijiji vya Shenda, Ipoja, na Buluhe. Mkusanyiko huu ulikuwa na watu wa kada
mbalimbali; walimu, wajumbe wa serikali ya kijiji, wazee, na wakulima.
Aliwakuta wakiwa pamoja na Mwenyekiti na Mtendaji wa kijiji chao. Na wote kwa
pamoja walikuwa wanazungumzia mustakabali wa maendeleo ya kijiji chao.
Na kwa
haraka aligundua wote wamekuwa waraghabishi, akajiuliza aliyekutana na Chukua
Hatua alikuwa mmoja, lakini sasa wapo kwa makundi na wote wanajitambulisha kama
waraghbishi.
Hamu na shauku yao ya
kutaka kusimamia rasilimali zao ndio imekuwa nguzo kubwa ya wao kuweza kufuatilia
matumizi ya vyanzo vya mapato ya kijiji chao.
Ni miaka miwili imepita toka
wananchi hao wautoe uongozi wa kijiji madarakani kwa tuhuma za ubadhirifu wa
fedha. Kwa pamoja waliongozana na mwenyekiti wao pamoja na mtendaji wa kijiji
na mpaka ofisi ya kata na kuwakabidhi kwa polisi.
Ubadhirifu huo ulithibitishwa
na taarifa ya ukaguzi, iliyoonyesha upotevu wa kiasi cha shilingi milioni mbili
laki tisa na elfu hamsini (2,950,000/-).
Taarifa hiyo ilisomwa katika mkutano
wa hadhara na viongozi kutakiwa kulipa pesa hizo ambazo walizirudisha.
|
![]() |
|
Waraghbishi
toka vijiji vya Iponya, Nyakasumula, Bukandwe na Shenda wakiwa katika pichaya
pamoja na mwenyekiti na mtendaji wa kijiji cha Shenda.
Baada ya
hapo walichagua uongozi mpya; mwenyekiti na halmashauri ya serikali ya kijiji
na Mkurugenzi wa wilaya akawaletea mtendaji mpya wa kijiji.
Na huo ndio ukawa
mwanzo mpya wa safari ya uraghbishi katika kijiji hicho. Vuguvugu hilo la
mapinduzi liliongozwa na waraghbishi wapya waliowezeshwa na Fedson wakisaidiana
na rafiki yake wa karibu Abdu Haridi ambaye pia ni mraghbishi.
Habari ya kutolewa madarakani kwa uongozi wa
kijiji hicho ilirushwa pia na redio ya Kahama FM na kupelekea mkuu wa wilaya
kumtuma mwakilishi wake akaongee na wananchi wa kijiji cha Shenda.
Uungwaji mkono huu na Mkuu wa Wilaya ni dalili
kwamba yupo tayari kufanyakazi na wananchi wa kijiji cha Shenda. Yeye ni
kiongozi wao na dhahiri anawajibika kwao kama ambavyo kiongozi yeyote anayejali
watu wake angefanya.
Kwa sasa
wanashirikiana kwa pamoja na uongozi mpya na mwandishi alithibitisha hivyo kwa
kuwa alipata fursa ya K a m a mwanzo
mpya, wamekubal i ana kufanya ujenzi wa ofisi mpya ya kijiji.
K wa n z
a wa meanza na ujenzi wa zahanati kwa k
u k a m i l i s h a msingi wake. Na wananchi wamekubali kuchangia, kila kaya
matofali 50 na wengine w a m e c h a n g i a mawe. Uhai umerudi tena na kila
mtu ana shauku ya kufanikisha ujenzi huo.
Lakinisi hivyo tu wanataka kukamilisha
pia na ujenzi wa zahanati ya kijiji. Haya yote yakiwa ni matunda ya ushirikiano
kati ya uongozi wa kijiji na waraghbishi na
wanakijiji wote kwa ujumla.
“Tumekaa muda mrefu sana bila zahanati hasa kwa ajili ya kina mama. Ni
kilometa tano kutoka hapa mpaka zahanati ya jirani. Na kijiji chetu kama
unavyokijua, hakina teksi, labda tumbebe kwa tela la ng’ombe au punda kama huna
baiskeli.
Tukajiuliza kwanini tusiiambie serikali yetu tujenge zahanati hapa
karibu,”anafafanua Abdi Haridi. Lakini
si hivyo tu Mwenyekiti ameshahamasisha kila mwananchi achangie mawe, achangie
matofali.
Kwa sasa wameonela kumalizia kabisa ofisi yao ya kijiji. Ya sasa ipo
katika hali mbaya harufu ya kinyesi cha popo na jengo lenyewe lina nyufa
ikinyesha mvua kubwa itakuwa ni shida inaweza hata kuanguka na hapa ndio makao
makuu ya kijiji.
Kwa hiyo nguvu zao sasa ni kukamilisha hii
ofisi afu ndio waendelee na zahanati ya kina mama. Mazungumzo hayo na Chukua Hatua yalifanyika
katika mfumo wa mafunzo yaliwawezesha
waraghbishi toka vijiji vya Ipoja, Shenda, Buluha na Nyakasaluma kuanza
kufuatilia na kuhamasisha wengine kufanya hivyo pia.
Si kitu kirahisi sana kuwa mraghbishi,
kunahitaji kujiamini, kujitambua na moyo wa kujitolea pia..
Katika kijiji cha Nyakasaluma wananchi
walihamasishwa na uongozi wao kuchangia pesa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati na
kwa kweli walichangia kila kaya ilitoa kiasi cha shilingi za kitanzania elfu
saba mia tano.
Swali la kujiuliza michango ya maendeleo ya namna hii,
inaamuliwaje? Wananchi wanahusishwaje? Je, wamefanya utambuzi wa
watu/kaya/familia uwezo walio nao?
Kwa mujibu wa mraghabishi Patrick Matagale
ujenzi ulianza lakini ghafla ukasimama na walipofuatilia ikaonekana kwamba
ujenzi hautaendelea kwa madai kwamba mwekezaji wa kijiji atamalizia na wananchi
pesa wameshachangia.
“Sasa ilikuwa ni kuhoji tu kuhusu ile pesa
iliyochangwa na wananchi”, anasimulia mraghbishi Patrick. Uaminifu ni silaha kubwa ya uongozi imara, na
mara watu wanaposhindwa kukuamini kama kiongozi, huamua kuchukua njia yao ya
kutokukupa dhamana ya kuwaongoza,
“Hivyo tulichoamua kufanya kwa sasa ni kwamba hatutachangia tena pesa na
badala yake tunahamasisha watu kuchangia vitu badala ya pesa, kama walivyofanya
wenzetu wa Shenda.
Mwenye mawe, matofali, mbao na chochote kile alete,”
anafafanua mraghbishi Patrick Matagale toka kijiji cha Nyakasaluma.
Katika kijiji cha Iponya, suala lililoibuka ni
michango wanayochangishwa wananchi. Ambapo kila kaya imetakiwa kuchangia kiasi
cha shilingi za kitazania elfu sita (6,000/) kwa ajili ya mradi wa maji wa
visima virefu.
Mradi huu unafadhiliwa na benki ya dunia na una thamani ya
shilingi za kitanzania milioni 221/-
Hivyo
wananchi nao wametakiwa kuunga mkono juhudi hizo kwa kuchangia pia gharama za
ujenzi huo na wananchi walikubali bila kusita na kwa ujumla wao walichangia
kiasi cha shilingi za kitanzania milioni tatu (3,000,000/-).
“Cha kushangaza wananchi wameshachanga hela
zao, ila mpaka muda huu naongea hakuna ambacho kimeshafanyika. Lakini kwenye
muhadhara tulidanganywa kwamba mradi ukishaanza Shenda na sisi pia tutaanza
kufaidika, mpaka dakika hii hakuna maji,” anafafanua Thomas Mlekwa toka katika
kijiji cha Iponya.
Wananchi wakawa
wanataka kujua nini kimetokea baada ya wao kuchanga, kama anavyosimulia mwana
mama Leornada Mathias toka kijiji cha Ipoja, “Ilikuwa mishe mishe kweli, kila
siku mwenyekiti anapita katika kaya anahamasisha watu wachangie ili tuondokane
na tatizo la maji.
Ni kweli
tuliitikia tukatoa michango na tuliambiwa tukichelewa tu huu mradi unatupita.
Tukafungua akaunti na fedha zikawekwa.
Baada ya hapo tukaona kimya kabisa.” Katika mikutano ya hadhara ya kijiji
iliyofanyika hapo wananchi walitaka kujua nini kimetokea kwani fedha tayari
kiasi cha shilingi za kitanzania milioni tatu zimeshawekwa benki.
“Kwenye
mkutano watu wakataka kujua meza imekuwaje tuliambiwa Shenda wakipata maji na sisi pia, mbona tayari kwa wenzetu
yapo. Ndio tukaja kujua kwamba hakuna mradi wa maji.
Na badala yake viongozi
wanatuambia kwamba ile fedha wanaanza kuisoma kwenye mapato na matumizi,”
anaendelea kufafanua Leornada.
Na katika muda huo wakaambiwa kwamba tayari
laki nne zimeshatumika kutokana na makato ya gharama za kuendesha akaunti. Kwa
hiyo uendeshaji wa akaunti umekula mpaka sasa kiasi cha milioni mbili na laki
tatu zimebaki laki saba tu.
Hapa pana kazi kubwa ya kufanya. Pamoja na Shenda kuonekana kwamba kwao maji
yameshaanza kutoka katika mabomba, bado kuna changamoto nyingi za kuwezesha
kukamilika kwa mradi huo wa maji.
Na waraghbishi wapo mstari wa mbele kufuatilia
nini kinachoendelea kwenye mradi huo. Ni mradi ambao waliomba wapatiwe na
utekelezaji wake umeshaanza ingawa baadhi ya maeneo bado hawapati maji.
“Mradi huu wa maji ni sawa na hakuna. Sisi
wananchi wa Shenda tumechangia nguvu zetu. Tumechangia asilimia yetu
tuliyoambiwa na serikali. Serikali ikachangia asilimia yake, ina maana kilikuwa
ni kisima tu cha vitongoji vine vya kijiji chetu. Tuna tenki lile pale
limeshakamilishwa. Mashine ipo kule
kwenye chanzo cha maji.
Italike kule, lakini kijiji kizima kuna gati nane tu.
Kuna vitongoji vingine havina gati. Kitongoji kizima kinapewa gati moja ebu
niambie kitakidhi wangapi?” anauliza Abdi Haridi mraghbishi wa Shenda.
Gati
zilizopo Shenda zinatokana na waraghbishi na wananchi kufuatilia suala hilo kwa
karibu.
Kwa sababu ni kitu walichokiomba wapatiwe na serikali. Baadhi ya
vitongoji vya kijiji hicho vimetenganishwa na barabara.
Hivyo wametaarifiwa
kwamba gati haiwezi kuvuka barabara. Ili hali kwa baadhi ya viongozi wao gati
imevuka barabara,” mraghbishi Abdi anauliza,
“Lakini ukienda pale makao makuu ya kata pale unakuta gati imewekwa kwa
kiongozi.
Nikauliza swali pale mbona kule Shenda tumeambiwa gati haiwezi kukata
barabara ndio maana wananchi wa upande wa pili wa kijiji hawapati maji.
Imekuwaje kwa kiongozi imekata barabara na kuingia mpaka mgongoni mwa nyumba
yake? Barabara ile ile niliyoambiwa gati haiwezi kukatiza ndio hiyo hiyo
imetumiwa kukatiza gati.” Kaloras Majura, mraghbishi kutoka kijiji cha Bukandwe
kutoka kata yenye jina hilo hilo la Bukandwe, pamoja na kwamba yeye ni
mraghbishi lakini pia alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi ya
kijiji chao.
“Changamoto niliyoanza nayo ilikuwa ni pale
shule, nilipogundua kwamba mwalimu mkuu anaitisha michango, bila kuwashirikisha
wazazi.
Pamoja na nafasi niliyokuwa nayo lakini pia nilikuwa natoa elimu kwa
wananchi. Nikajengewa kampeni na kufanyiwa uhasama na mwisho wa siku nikaambiwa nafasi ya uenyekiti
hainifai, kwa sababu natoa siri.
Hivyo nimebaki mjumbe tu,” katika hali ya
upole anaelezea mraghbishi Majura.
Suala
lingine ambalo limejitokeza ni kuhusu mganga wa zahanati ya kijiji cha
Bukandwe, ambaye alikuwa akiwachangisha wananchi kiasi cha shilingi za
kitanzania elfu kumi (10,000/-) za mfuko wa afya.
Alichokuwa akifanya wakati
anawaandikia alikuwa akiweka kumbukumbu tofauti za mwaka. “Kama mtu katoa hela mwaka huu yeye
anamuandikia katoa mwaka 2012 na wengine mwaka 2013.
Baada ya muda akawa
amehamishwa sasa watu wanapokwenda pale zahanati wanaambiwa kwamba wewe muda
umeshakwisha ulitoa mwaka juzi hivyo uanze upya,” anasimulia Majura Kutokana na nafasi yake ya uraghbishi Majura
ameweza kukaa na kamati ya kijiji ya afya.
Na ameishawishi kamati kuwasiliana
na watu waliolipa kuandaa vielelezo vyao na kufanya mawasiliano na mganga mkuu
wa wilaya, ili waweze kujua wanachukua hatua gani kuhusu huyo mganga. Lengo la
kufanya hivyo ni kuhakikisha kwamba wananchi wanarudishiwa fedha zao
walizochanga.
Si kitu
kirahisi sana pia kufanya uraghbishi kwa sababu mara kadhaa waraghbishi
wamekuwa wakitishiwa tishiwa ili wasiulize ulize maswali na kuhamasisha
wananchi , lakini bado mambo
yameendelea. “Sisi waraghbishi tunapata
muda mgumu sana tunakutana na watu tofauti na viongozi tofauti.
Tunatishiwa
amani, ila na sisi tutapambana kama tulivyokwisha kupambana mpaka dakika ya
mwisho ili haki yetu ipatikane. Tukianza kuyatafuta mashirika ili tushirikiane
nayo katika kuweka mambo sawa, kama hivi.
Tayari tunaonekana siye wabaya kwa
wale viongozi wa juu. Kwamba sisi tunawapondea wale. Basi sisi tunaomba waje wale
wakubwa zaidi, waje watuulizie nini kinaendelea ili tuwaambie ukweli,” anaeleza
kwa kujiamini mraghbishi Abdi Haridi wa Shenda.
Harakati hizi zinaungwa mkono na mwenyekiti
wa kijiji cha Shenda, Masumbuko Kwileka, kama anavyosema kuhusu warghabishi,
“Kila siku waraghbishi tunao hapa. Fedson huwa
anakujaga hapa wanazunguka huko na kijana wake huyu hapa Haridi. Wanapita
vijiji hadi vijiji wanahamasisha.
Hivyo waraghbishi wana hamasa hata mwenyekiti
ajaye atakayekuja watakuwa msaada kwake. Manake watamuuliza tu sasa mkuu
unakwendaje hapa na itabidi uwaeleze mambo yanakwendaje.
Hivyo mnapopata pesa
ni lazima umuelezee mraghbishi zinavyokwenda.”
Ni mwaka sasa umepita toka shuguli za Chukua Hatua zisimame kwa muda, ila
cha kufurahisha ni waraghbishi wameendelea na harakati za kujiletea maendeleo
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hasa wananchi wenzao.
Na si hivyo tu
wameendelea kuwatengeneza waraghbishi wengine ambao na wanaendeleza harakati za
kuleta maendeleo.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|







No comments:
Post a Comment