|
Manchester
United wametoka sare ya 0-0 na West Ham kwenye mchezo wa Ligi kuu jioni ya leo
Desember 05,2015 na matokeo haya yanatia presha sasa Kocha wa Man United Louis
van Gaal kuwa huenda taondoka klabu hapo zimekuwa zikichukua nafasi kila siku,
kwani mashabiki wa timu hiyo hawana imani na uwezo wa kocha huyo tena, baadhi
ya wachezaji wanahusishwa kuwa hawauelewi mfumo wa kocha huyo ukilinganisha na
wakati ambao yupo Sir Alex Ferguson.
Habari za
Van Gaal kuhusishwa kufukuzwa kazi zimekuwa zikiandikwa ila December 5 kabla ya
mchezo kati ya Man United dhidi ya West Ham United Louis van Gaal katoa majibu
ya kuhusu hatma yake ndani ya Man United.
Van Gaal
yupo radhi kuondoka Man United endapo tu wachezaji wataamua aondoke.
“Mimi ndiye
kocha wa kwanza ambaye huwa naachia ngazi na hilo linathibitisha kupitia klabu
nilizofundisha pia kazi nilizozifanya, sidhani kama kuna kocha yeyote ambaye
huwa anaondoka mwenyewe tu au sababu ya pesa, ila mimi nipo hivyo”>>>
Van Gaal.
|
No comments:
Post a Comment