EPL 2015/2016:-Pichani Arsenal 2-1 Manchester City ,goli za Theo Walcott na Olivier Giroud. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, December 22, 2015

EPL 2015/2016:-Pichani Arsenal 2-1 Manchester City ,goli za Theo Walcott na Olivier Giroud.

Mabao mawili yaliyofungwa na Theo Walcott pamoja na Olivier Giroud yameiwezesha Arsenal kuibuka na pointi 3 kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Manchester City  kwenye mchezo uliochezwa usiku wa Jumatatu December 21,2015  wa Ligi Kuu Uingereza 2015/2016 , mchezo uliomalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Arsenal walipata goli la kwanza likifungwa dakika ya 33 na Walcott wakati Giroud yeye alipiga la pili dakika ya 45.

Yaya Toure alifanikiwa kuipatia timu yake bao la kufutia machozi dakika ya 82 kipindi cha pili kwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na beki wa kulia wa timu hiyo Sagna.

Matokeo hayo yanawafanya The Gunners kufikisha pointi 36 ponti mbili nyuma ya vinara wa ligi hiyo Leicester City ambao wanaongoza ligi wakiwa na pointi 38 huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 17 hadi sasa. Manchester City bado wataendelea kusalia kwenye nafasi ya tatu wakiwa na pointi zao 32 nyuma ya Arsenal.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad