EPL 2015/2016:- Hiki ndicho Newcastle wamekitoa kwa Liverpool usiku huu wa leo December 06,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 06, 2015

EPL 2015/2016:- Hiki ndicho Newcastle wamekitoa kwa Liverpool usiku huu wa leo December 06,2015.

 Newcastle usiku huu wa leo December 06,2015  wamepata ushindi wao wa 3 kwenye Ligi Kuu Uingereza Msimu huu 2015/2016 walipoitwanga Liverpool 2-0 kwenye uwanja wao wa Saint James Park.

Martin Skrtel alijifunga mwenyewe katika Dakika ya 69 katika harakati za kuokoa bomba la Georginio Wijnaldum.

Newcastle walipiga Bao la pili Dakika ya 93 wakati Bango likiashiria Dakika 5 za nyongeza kufuatia kazi nzuri sana ya Moussa Sissoko kwenye Winga ya Kulia aliemlisha Wijnaldum aliemchambua Kipa Mignolet na kuamsha shangwe Uwanjani Saint James Park.

Ushindi huu umewainua Newcastle hadi Nafasi ya 18 wakiwa Pointi 1 juu ya Timu ya 19 Sunderland na Pointi 7 mbele ya mkiani Aston Villa.

Liverpool wamebaki Nafasi ya 7 wakiwa na Pointi 23 zikiwa ni Pointi 6 nyuma ya Timu ya 4 Man United.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad