AJALI / PICHA:-Ajali ya basi igunga Mtu mmoja afariki, 38 wajeruhiwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 21, 2015

AJALI / PICHA:-Ajali ya basi igunga Mtu mmoja afariki, 38 wajeruhiwa.

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 38 kujeruhiwa baada ya Basi la Allys Coach lenye namba za usajili T 560 AKM lililokuwa likitokea Igunga,Mkoani Tabora  kuelekea Mwanza kuyumba na kuanguka katika kijiji cha Igogo kata ya Nanga wilayani Igunga Mkoani Tabora.

Ajali hiyo imetokea December 20,2015, majira ya saa 12 na nusu asubuhi na chanzo chake kikidaiwa kuwa ni mwendo kasi wa dereva kutaka kulipita gari la mizigo.

Ajali hizi zimekuwa zikigharimu maisha ya watu na wengine kuwaachia ulemavu wa kudumu,sababu zikielezwa ni mwendo kasi wa baadhi ya madereva na kutozingatia sheria za barabarani, baadhi ya majeruhi wa ajari hii wanaeleza hali ilivyo kuwa.
Baadhi ya majeruhi wameiomba serikali kusimamia sheria ikiwa na abiria kufunga mikanda na kudhibiti mwendo kas.

Aliyepoteza maisha katika ajari hiyo ni Denis Sokolo (34) mkazi wa Igunga na hapa mganga mkuu mfawidhi wa Hospital ya wilaya ya Igunga Merchadeth magongo anathibitisha kupokea majeruhi na hali zao kwa pamoja.

Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa ajari hiyo na uchunguzi unaendelea.

 Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

Post Bottom Ad