R . I . P KAMANDA MAWAZO:-Lowassa, Mbowe, Sumaye watua alipouawa Mawazo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, November 30, 2015

R . I . P KAMANDA MAWAZO:-Lowassa, Mbowe, Sumaye watua alipouawa Mawazo.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe  na aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Ukawa, Edward Lowassa, pamoja na viongozi mbalimbali wakitazama eneo ambalo Alphonce Mawazo, huku wakiamini kifo hicho kilipangwa kutokana na kushambuliwa eneo la wazi katika barabara kuu ya Geita - Katoro.

 Msafara wa Lowassa ukiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, wakiwa na wabunge zaidi ya 50 na wanachama na wafuasi wa chama hicho, walienda eneo hilo lililopo  jirani na makazi ya watu na kujioneo hali halisi.

Mwili wa marehemu Alphonce Mawazo, unatarajiwa kuzikwa leo,Jumatatu November 30,2015,kijijini kwao Chikobe, wilayani Geita,mkoani Geita.

Marehemu Mawazo aligombea  Jimbo la Busanda alilowania ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu,2015  na kushindwa.

Aliuawa Novemba 14, mwaka huu ,2015 na watu wasiojulikana katika mji wa Katoro.
 
Umati mkubwa wa wakazi wa Jimbo la Busanda waliojitokeza kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mgombea Ubunge na Mwenye kiti wa Mkoa wa Geita, Marehemu Alphonce Mawazo.

Mwili wa Marehemu Alphonce mawazo ukipokelewa na wakazi wa jimbo la Busanda ambako alikuwa akiwania Ubunge katika jimbo hilo.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad