MAHAKAMANI:-Sheikh Ponda Aachiwa Huru . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, November 30, 2015

MAHAKAMANI:-Sheikh Ponda Aachiwa Huru .

Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia.

Makosa yaliyokuwa yakimkabili ni mawili ambayo ni kushawishi watu kutenda kosa, pamoja na kutoa matamshi yanayoumiza imani ya dini nyingine.

Hakimu wa kesi hiyo Mary Moyo amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haukujitosheleza hivyo mahakama hiyo imemwachia huru na rufaa iko wazi endapo upande wa mashitaka hautaridhika na hukumu hiyo.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad