MAFANIKIO YETU:-Mo apata tuzo nyingine, adhihirisha tamaa ya kuwatumikia watanzania.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, November 30, 2015

MAFANIKIO YETU:-Mo apata tuzo nyingine, adhihirisha tamaa ya kuwatumikia watanzania..

Mfanyabiashara maarufu ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji katika Ubora wake Pichani akitunukiwa tuzo ya "Forbes Africa Person Of the Year 2015".(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Mfanyabiashara na  mtu mwenye taasisi ya kusaidia jamii, Mohammed Dewji maarufu kama Mo ametunukiwa tuzo ya jarida maarufu la Forbes ya  "Forbes Africa Person Of the Year 2015" katika hafla iliyofanyika Novemba 27 mwaka huu,2015 jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

 Mfanyabiashara huyo pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises T Ltd (MeTL Group) kampuni iliyoanzishwa na na baba yake katika miaka ya 1970 ambayo sasa imekua na kujikita katika viwanda vya nguo, usagaji nafaka, utengenezaji wa vinywaji baridi, usindikaji wa mafuta ya kula, usindikaji wa chai  na kuendesha mashamba ya mkonge ambapo tayari anashea ya asilimia 40 ya soko.

Mwanzilishi na mchapishaji wa jarida la Forbes Afrika, Bw. Rakesh Wahi ( wa pili kushoto)  akikamkabidhi Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji (wa pili kulia) tuzo ya Mtu wa Mwaka “2015 Forbes Africa Person of the Year”  iliyotolewa na Jarida la Forbes Afrika kwa kutambua mchango wake katika kusaidia jamii ikiwemo kutoa ajira kwa zaidi ya watu 26,000 nchini na mambo mengine yanayoigusa jamii. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Forbes Afrika, Sid Wahi (kulia) na MEC Panyaza Lesufi kutoka kitengo cha elimu, Gauteng Province (kushoto).(Picha hii kwa hisani ya Helenus Kruger).

MO katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Makampuni ya MeTL Group, Vipul Kakad mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.


Mo ametwaa tuzo hiyo kwa kuwashinda watu watano mashuhuri barani Afrika. Watu hao ni Nkosazana Dlamini Zuma, mke wa Kwanza wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma. Mama huyo kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU). Mwingine ni Rais wa sasa wa Nigeria, Muhammadu Buhari aliyetambuliwa kutokana na kuanzisha vita dhidi ya rushwa nchini mwake.

Aidha wapo Arumna Otei, mchumi mahiri raia wa Nigeria ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia. Pia alikuwemo Mwandishi maarufu wa vitabu wa Nigeria, Chimanda Ngozi Adichie ambaye moja ya vitabu vyake vinaelezea picha halisi ya Afrika inavyofikiriwa duniani.

Akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa kwa tuzo hiyo Mo, alisema anatoa tuzo hiyo kwa vijana wa Kitanzania kwani ndio nguvu kazi inayobeba uchumi wa nchi.

Mo ambaye kampuni yake ya MeTL inaongoza kwa kutoa ajira nchini, ikiwa imetoa ajira 26,000 kote katika viwanda vyake 31 vilivyopo nchini na katika mataifa matano ya Afrika, alisema amefurahishwa na tuzo hiyo ambayo anaitoa kwa vijana kwa kutambua pia wajibu mkubwa walionao katika kukabiliana na umaskini. BOFYA HAPA KUSOMA NA KUTAZAMA PICHA ZAIDI.
Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na Shemane Amin wakipitia moja ya taarifa iliyowavutia kwenye jarida la Forbes Afrika.
MO katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Jaguar Land Rover ambao ni miongoni mwa wadhamini wa sherehe za tuzo hizo.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad