EPL 2015/2016:-Tazama Matokeo ya mechi za November 28,2015 na rekodi iliyovunjwa na Jamie Vardy . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 29, 2015

EPL 2015/2016:-Tazama Matokeo ya mechi za November 28,2015 na rekodi iliyovunjwa na Jamie Vardy .

Mshambuliaji wa Leicester, Vardy amevunja rekodi baada ya kufunga mfululizo katika mechi 11 za Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu wa 2015/2016.
Jamie Vardy kavunja rekodi ya Ruud Van Nistelrooy baada ya kufunga goli katika mechi 11 mfululizo. Goli la kufikisha safari ya mechi 11 mfululizo akifunga limekuwa dhidi ya timu ya zamani ya Nistelrooy yaani Manchester United akifunga katika kipindi cha kwanza.

Mchezaji Ruud Van Nistelrooy aliweka rekodi ya awali kwa michezo ya misimu miwili ya mwaka 2003. Mpaka anavunja rekodi hii Vardy amefunga magoli 13 katika kipinid hiki huku pia akiwa amefunga magoli 14 na kuongoza orodha ya wafungaji ligi kuu ya Uingereza.

Mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Leicester City, Ngolo Kante.

Manchester United wametoka sare 1-1 na Leicester City na matokeo haya kuiruhusu Manchester City kutwaa uongozi wa Ligi Kuu Uingereza 2015/2016 baada ya Manchester City kuichapa Southampton 3-1 .

Katika mchezo wa Man City, magoli yao yalifungwa na Kevin de Bruyne, Fabian Delph na Aleksandar Kolarov wakati Southampton walipata Bao lao kutoka kwa Shane Long.

Jumamosi Novemba 28,2015.

Aston Villa 2 – 3 Watford  
           
Bournemouth 3 – 3 Everton  
        
Crystal Palace 5 – 1 Newcastle 
              
Man City 3 – 1 Southampton  
               
Sunderland 2 – 0 Stoke 0  
             
Leicester 1 – 1 Man United   
         
Leicester walitangulia kufunga kwa bao la Jamie Vardy katika Dakika ya 24 na kumfanya avunje rekodi ya Mchezaji wa zamani wa Man United, Ruud Van Nistelrooy, aliyoiweka Mwaka 2003 ya kufunga katika Mechi 11 mfululizo za Ligi Kuu.

Manchester  United walisawazisha katika Dakika ya 45 kwa Bao la kichwa la Bastian Schweinsteiger.

Jumapili Novemba 29,2015.

1500 Tottenham v Chelsea  
           
1705 West Ham v West Brom 
        
1915 Liverpool v Swansea  
            
1915 Norwich v Arsenal
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad