CECAFA CHALENJI CUP 2015: SAFU ROBO FAINALI:-Tanzania bara kuchuana na wenyeji Ethiopia. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 29, 2015

CECAFA CHALENJI CUP 2015: SAFU ROBO FAINALI:-Tanzania bara kuchuana na wenyeji Ethiopia.


Hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge CUP 2015 inahitimishwa November 28, 2015 kwa michezo miwili.

Mechi nyingine za mwisho za makundi zilichezwaNovember 27,2015, Zanzibar ikiifunga Kenya mabao 3-1, wafungaji, Suleiman Kassim 'Selembe' mawili na Khamis Mcha 'Vialli' moja, wakati bao la Harambee Stars lilifungwa na Jacob Keli, Rwanda imeifunga 3-0 Somalia, wakati Sudan Kusini iliifunga 2-0 Malawi,Sudan iliifunga Djibouti 4-0.

Tanzania Bara, maarufu Kilimanjaro Stars, ilitoka Sare na wenyeji Ethiopia Bao 1-1 na kumaliza Kundi A wakiwa Washindi wa Kundi hilo na sasa watacheza na Ethiopia kwenye Robo Fainali.

Bao la Stars , lilifungwa na Simon Msuva Dakika ya 51 na Ethiopia kusawazisha Dakika ya 90 kwa Bao la kujifunga wenyewe la Salum Mbonde.

MECHI ZA MWISHO ZA MAKUNDI



Ijumaa Novemba 27,2015.

Rwanda 3 – 0 Somalia 

Zanzibar 3 – 1 Kenya 

South Sudan 2 – 0  Malawi 

Djibouti 0 – 4 Sudan

Jumamosi Novemba 28,2015.

Uganda 1 – 0 Burundi 

Tanzania 1 – 1  Ethiopia

RATIBA ROBO FAINALI CECAFA CHALENJI CUP 2015.


Jumatatu Novemba 30, 2015.

Uganda Vs Malawi

Tanzania Bara Vs Ethiopia  

Jumanne Desemba 1, 2015.

Sudan Kusini Vs Sudan

Rwanda Vs Kenya


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad