VPL 2015/2016:-Simba yaipa 6 - 1 Maji Maji FC na matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu October 31,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 31, 2015

VPL 2015/2016:-Simba yaipa 6 - 1 Maji Maji FC na matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu October 31,2015.


Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea tena leo October 31,2015  kwa Timu ya Simba SC kucheza na  Maji Maji FC kutoka,Ruvuma Songea. 

Katika mchezo huo , Mshambuliaji  Ibrahim Hajib ‘Kadabra’ amefunga mabao matatu peke yake, Simba SC ikishinda  6 -1 dhidi ya Majimaji ya Songea katika mchezo wa Ligi Kuu  jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 Hiyo inakuwa hat trick ya pili katika Ligi Kuu msimu huu na zote zikitoka Simba SC, baada ya awali Mganda Hamisi Kizza kufanya hivyo.

Na ushindi huo, unaifanya timu ya kocha Muingereza Dylan Kerr ifikishe pointi 21 baada ya kucheza mechi tisa, ikiendelea kushika nafasi ya nne nyuma ya Yanga SC, Azam FC na Mtibwa Sugar.
DSC_0185

DSC_0216
Magoli ya Simba SC yalifungwa na Ibrahim Ajib aliyefunga hat-trick kwa kuanza kufunga goli la kwanza dakika ya 8, 14 na 42 akakamilisha idadi ya goli zake tatu, Hamisi Kiiza alifunga goli mbili katika mchezo huu dakika ya 32 na dakika ya 81 baada ya dakika ya 71, Hussein Mohamed ‘Tshabalala‘ kufunga goli la tano kwa Simba, Maji Maji FC walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa Ditram Nchimbi.

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu October 31,2015.

          Kagera 0 – 2 Yanga SC 

          Coastal Union 1 – 1 Mbeya City

          Mtibwa Sugar 4 – 1 Mwadui FC
DSC_0317
DSC_0152
DSC_0179
DSC_0325
Simba ndio timu pekee mpaka sasa ambayo imetoa wachezaji waliofunga magoli matatu kwenye kwenye mechi moja (hat-trick) msimu huu ambao ni Hamis Kiiza na Ibrahim Ajib.
DSC_0137
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad