FUNUNU NA TETESI:-Lembeli aeleza hatma yake baada ya kushindwa Ubunge. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 31, 2015

FUNUNU NA TETESI:-Lembeli aeleza hatma yake baada ya kushindwa Ubunge.

Lembeli aeleza hatma yake baada ya kushindwa Ubunge
Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama, Bw.James Lembeli ameelezea kinachoendelea katika maisha yake ya kisiasa hasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu akiwa ndani ya chama chake kipya cha CHADEMA.

 Akiongea katika taarifa rasmi kwa wananchi wa jimbo Kahama, Lembeli amesema kuwa hivi sasa atajikita zaidi katika shughuli za chama chake pamoja na shughuli alizokuwa akizifanya kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Alisema kuwa ataendelea kufanya kazi zake na mashirika ya kimataifa kama mjumbe wa Bodi mbalimbali. Pia, ataendelea kufanya kazi ya kusimamia radio yake (Kahama FM) ambayo amedai kuwa taarifa zilizosambazwa kuwa ameiuza kulipa deni la mkopo aliopewa kuendesha kampeni sio za kweli.

Pia, Lembeli amewashukuru wananchi waliojitokeza kumuunga mkono na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika masuala ya maendeleo na ataendeelea kushirikiana nao kukamilisha miradi mbalimbali aliyokuwa ameanza kuitekeleza kwa juhudi zake binafsi.

Kadhalika, Lembeli amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kuwa alikamatwa na jeshi la polisi mara tu baada ya Jumanne Kishimba wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.

Kuhusu afya yake, alisema kuwa yeye ni mzima tofauti na habari zinazoendelea kuenea kuwa ni mgonjwa hasa baada ya kupata ajali ya gari na matokeo kutangazwa.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad