VIPAJI VYETU:-Tazama Picha wakati Kayumba Juma akiibuka Mshindi wa Shindano la Bongo Star Search 2015 (BSS) na kutwaa Sh 50 milioni. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 11, 2015

VIPAJI VYETU:-Tazama Picha wakati Kayumba Juma akiibuka Mshindi wa Shindano la Bongo Star Search 2015 (BSS) na kutwaa Sh 50 milioni.

1

Mshindi wa Shindano la Bongo Star Search 2015 (BSS), Kayumba Juma (katika), akiwa ameshikilia fedha zake muda mfupi baada ya kuibuka kidedea kwenye fainali hizo zilizokuwa zikifanyika usiku wa kuamkia October 10,2015, katika Ukumbi wa King Solomoni uliopo Namanga jijini Dar es Salaa.


2

Jaji Mkuu wa mashindano hayo, Madam Rita (wa pili kutoka kushoto), akimtangaza mshindi huyo.
3

Washiriki waliongia kwenye 6 bora ya mashindano hayo wakiwa jukwaani kabla ya mchujo huo kuanza
5

Majaji wakiwa kwenye meza yao ya kuratibia mashindano hayo.

7

Wasnii wanaounga kundi la Navy Kenzo wakipagawisha jukwaani hapo.

8

Msanii kutoka nchini Nigeria, Run Town anayetamba na kibao chake cha Gallardo, akipagawisha jukwaani hapo.

9

Mmoja wa washiriki waliokuwa wakichuana jukwaani hapo, Angel Marykato akisaka milioni 50.

10

Vijana wanaounda kundi la Yamoto Bendi wakitoa burudani kwenye fainali hizo.

11

Msanii wa Dansi Christiani Bella akitunza na mashabiki wake wakati akitumbuiza kwenye fainali hizo.

12

Bosi anayesimamia lebo ya Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akishuhudia kwa makini fainali hizo.

13

Mshiriki wa Shindano hilo kutoka Arusha, Frida Amani akipagawisha jukwaani hapo kuwania kitita cha shilingi milioni 50.
14

Kala Jeremiah akikumbushia enzi zake katika mashindano hayo.
19

Kayumba akitunzwa na mashabiki wake kabla ya kutangazwa kuwa mshindi.

20

Madam Rita akifuta machozi muda mfupi baada ya kumkabidhi mshindi kitita cha shilingi milioni 50.

22

Mmoja ya kikundi cha kudansi kikitumbuiza jukwaani hapo.

24

Baadhi ya mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo wakifuatilia burudani hizo kwa makini.

Kayumba Juma wa jijini Dar es Salaam usiku wa October 09,2015 aliibuka mshindi wa shindano la kusaka vipaji vya muziki la Bongo Star Search (BSS) kwa mwaka 2015 baada ya kuwabwaga washiriki wengine watano waliofika hatua ya fainali, hivyo kutwaa kitita cha Sh50 milioni.

Mbali na kuondoka na fedha hizo, kijana huyo amepewa bima ya afya ya mwaka mzima kutoka kwa kampuni ya Jubilee Insurance.

Kayumba Juma aliibuka kidedea katika fainali hizo zilizofanyika katika Ukumbi wa King Solomon Hall, Kinondoni jijini Dar es Salaam zilizopambwa na wasanii mbalimbali wa muziki.

Mshindi huyo aliwabwaga washiriki wengine watano ambao walifika hatua ya fainali; Frida Amani, Nassib Fonabo, Jacqueline Kayengi, Angel Mary Kato na Kevin Gerson. Licha ya kushindwa kutwaa taji hilo washiriki hao watano walitoa ushindani mkubwa na kuwapa burudani mashabiki waliohudhuria kwenye ukumbi huo.

Sambamba na burudani kutoka kwa washiriki hao, pia wapo baadhi ya wasanii waliolipamba jukwaa la fainali hizo ikiwa ni pamoja na Kala Jeremiah, Peter Msechu, Christian bella, Yamato Band pamoja na msanii kutoka Nigeria, Runtown.

Jaji kiongozi wa mashindano hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark, Rita Poulsen alimtangaza mshindi huyo baada ya washiriki wote sita kuchuana jukwaani na kubaki wawili.

Baada ya wawili hao, Kayumba Juma akiwakilisha Dar es salam na Nassib Fonabo kutoka Arusha ambao waliingia katika hatua ya mbili bora na kutupa karata yao ya mwisho kwa kuimba muziki wa mwisho, mashabiki walipiga kura na muda mfupi baadae Jaji huyo maarufu kwa jina la Madam Rita alipanda jukwaani na kumtangaza mshindi.

Mnamjua mshindi…? Sina maneno mengi maana kazi yangu ni kumtangaza mshindi wa mashindano ya BSS msimu wa 8 (season eight), mshindi ni.. ni.. Kayumba Juma’’ alitangaza Madam Ritah huku mashabiki wakishangilia kutokana na burudani aliyotoa mshindi huyo. 

Mashindano hayo yanayoandaliwa na Kampuni ya Benchmark Production 360 yalianza mwaka 2006 kwa kusaka vipaji vya vijana wa Kitanzania kila mwaka lakini mwaka jana mashindano hayo hayakufanyika tofauti na ilivyozoeleka.

Baadhi ya washindi wa BSS kwa miaka tofauti toka shindano lianzishwe ni pamoja na; Jumanne Iddi, Kala Jeremiah, Peter Msechu, Walter Chilambo na Emmanuel Msuya.

Habari/Picha: Musa Mateja/GPL.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad