UCHAGUZI MKUU TANZANIA :- Ufafanuzi wa Idadi ya Vituo vya Kupigia Kura October 25,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 11, 2015

UCHAGUZI MKUU TANZANIA :- Ufafanuzi wa Idadi ya Vituo vya Kupigia Kura October 25,2015.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Kailima Ramadhani  amefafanua jinsi mabavyo Tume ya taifa ya uchaguzi ilivyo gawanya vituo vya wapiga kura kote nchini. 


Katika ufafanuzi huo amefafanua mambo makuu Mawili.


1. Namna ambayo siyo sahihi ya kuhesabu vituo vya wapiga KURA kama walivyo fafamua baadhi ya watu, Ambayo ni namna ya KUPOTOSHA NA NI UWONGO, na

2. Namna SAHIHI  ya kuhesabu vituo kama tume ye taifa ya uchaguzi ilivyo hesabu. Nia hii inazingatia mambo yafuatayo.

i). KUTUO HAKITAZIDI WATU 450

ii). KITUO KINAWEZA KUWA NA IDADI CHINI YA WATU 450

ILI WATU WALIOJIANDIKISHA KITUO KIMOJA WASIHAMISHWE KWENDA KUJAZIA ENEO JINGINE.

Itakuwa hivi.

Endapo kuna eneo ambalo watu waliojiandikisha ni 1900 Tume ya taifa ya uchaguzi itagawanya watu kama ifuatavyo:-

450+450+450 = 1300

1900-1300 = 550

550 gawanya kwa 2 = 275.


KWA HIYO MAHALI PENYE WAPIGA KURA 1900

PATAKUWA NA VITUO VITANO (5).


1. KITUO CHA KWANZA WATU 450

2. KITUO CHA PILI WATU           450

3. KITUO CHA TATU WATU        450

4. KITUO CHA NNE WATU          275

5. KITUO CHA TANO WATU       275

JUMLA                                            1900



ZINGATIA

Kutokana na kuwepo kwa vituo vyenye idadi ya watu chini ya 450 kumefanya idadi ya vituo iwe kubwa.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad