Taswira ya
Bango lenye picha ya Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa, likiwa kwenye mkutano wa
kampeni Namanga, Jimbo la Longido, jana October 7,
2015, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha .
Edward
Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Namanga, Jimbo la Longido,amewataka
Watanzania kujifunza kuchangamkia fursa
za ajira zinazotolewa na Afrika Mashariki kama ilivyo kwa nchi nyingine.
Pia Edward Lowassa ameahidi kuboresha huduma
za kibiashara katika maeneo ya mipakani ili kurahisisha biashara tofautina
ilivyo hivi sasa.
Lowassa
alisema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
atahakikisha kuwa watanzania wanachangamkia fursa za Afrika Mashariki kama
ilivyo kwa Kenya.
“Napenda
mahusiano ya Afrika Mashariki yawe ya kweli na siyo upande mmoja unafaidi na
mwingine haufaidi,”alisema na kuongeza kuwa:
“Watanzania
wakiwa wanapita kwenye mpaka wa Namanga wasisumbuliwe wapite bila shida.”
|
No comments:
Post a Comment