KURA YANGU 2015:-Tume ya Uchaguzi Tanzania NEC imetoa majibu kuhusu Wanafunzi kushiriki Uchaguzi Mkuu 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, October 08, 2015

KURA YANGU 2015:-Tume ya Uchaguzi Tanzania NEC imetoa majibu kuhusu Wanafunzi kushiriki Uchaguzi Mkuu 2015.

Tukiwa bado tupo kwenye headlines za Uchaguzi 2015 ,Hapo Jana Octoba 7, 2015 Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva ametolea majibu kuhusu Wanafunzi kushiriki Uchaguzi mkuu.

 ‘Suala la Wanafunzi mara kwa mara limekuwa likiletwa na sisi kwenye tume tumesema kwamba linafanywa kama la kisiasa kwa maana kwamba mara kadhaa wanafunzi walipokuja pale ofisi za tume kile kikundi chao  wakatuambia kwamba kipindi hiki watakuwa likizo‘ Lubuva.
.
Tukawapa ushauri na tukazungumza nao nimeenda mpaka chuo cha Dodoma tukazungumza nao na tukawapa utaratibu mpaka tukaunda kamati ikaongozwa na Jaji Mkwawa wasikilizwe wakaelezwa na baadae wakaandikiwa barua kwa hiyo hili suala ni   suala la kisiasa na tumeshughulika nalo  mwisho tukawaambia kwamba wamejinyima wenyewe  hii nafasi’- Lubuva.

LUBUVAA22
Kwa hiyo suala la wanafunzi ninasema kwa niaba ya wenzangu kwamba kwenye tume tumefunga mlango na upande wa kuboresha daftari umepita ni wao wenyewe wamejinyima na kuhusu kwamba vyuo vifungwe  kwasababu ya Uchaguzi Mkuu ni suala la Wizara ya Elimu sio la tume ya Uchaguzi – Lubuva.

Habari kwa hisani ya MILLARDAYO.COM



Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad