TANZIA:-RIP Mchungaji Christopher Mtikila…tayari umeagwa Dar, safari imeanza kwa ajili ya Mazishi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, October 07, 2015

TANZIA:-RIP Mchungaji Christopher Mtikila…tayari umeagwa Dar, safari imeanza kwa ajili ya Mazishi.

Asubuhi ya  Octoba 04 2015 taarifa ya Majonzi ilitufikia ambapo taarifa yenyewe ilikuwa inahusu msiba wa aliyekuwa Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha  DP, Christopher Mtikila ambaye alifariki kwa ajali ya gari eneo la Msolwa, Chalinze Mkoa wa Pwani.

Mwili wa Marehemu umeagwa leo October 07 2015 kuelekea mkoani Njombe na watu mbalimbali wamejitokeza kuaga mwili wa Marehemu katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam wakiwemo Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal pamoja na viongozi wengine wa Serikali na wanasiasa pia.
Jeneza la mwili wa Mchungaji Mtikila likishushwa viwanja vya Karimjee kwa kuagwa.

Rai wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete akisaini katika kitabu cha maombolezo.

Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisaini kwenye kitabu cha maombolezo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari, Maalim Seif Hamad Sharif akisaini kitabu cha maombolezo.

Rais Kikwete (katikati) akiwa kwenye msiba huo kabla ya kuuaga mwili wa Mch.Christopher Mtikila sambamba na viongozi wengine.

Waombolezaji wakihuzunika wakati wa kuuaga mwili…KWAPICHA ZAIDI BOFYA.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wake, Dk. Mohammed Gharib Bilal na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Hamad wamejitokeza leo kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kutoa heshima zao mwisho kwenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Democratic Party, Mchungaji Christopher Mtikila.

Marehemu Mtikila alikuwa mwanasiasa mkongwe aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Oktoba 4 mwaka huu katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze  Mkoa wa Pwani, wakati akirejea Dar es Salaam kutokea Njombe alikokuwa amekwenda kufanya mkutano wa kampeni.

Viongozi wa vyama vya siasa, taasisi na mashirika mbalimbali yalipata fursa ya kutoa shukurani zao za pekee kuzungumzia historia ya marehemu enzi za uhai wake ambapo kila mmoja alimzungumzia  Mchungaji Mtikila alivyokuwa kiongozi shujaa, mwenye maamuzi na kusimamia kile alichokuwa akikiamini.

Akitoa salamu za rambirambi Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Jaji, Francis Mutungi amesema kuwa marehemu ameacha pengo kubwa kwa chama cha DP, kwani alikuwa kiongozi aliyekuwa akisimamia haki na kile alichokuwa akiamini na alikuwa hapindishwi na mtu yeyote na alikuwa ni mmoja wa wanaharakati wa haki za binadamu.

Alisema kuwa Mtikila alikuwa mwanaharakati asiyependa maandamano mwenye kuchukua maamuzi ya kwenda mahakamani kwa ajili ya kupata haki anayoitaka na ndiye alikuiwa mwanzilishi wa kudai mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Mwili wa marehemu umesafilishwa kwenda Ludewa, Njombe ambapo wakazi wa mkoa huo watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuzikwa. Anatarajiwa kuzikwa kesho.

NA DENIS MTIMA/GP


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.   

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad