KAMPENI URAIS CCM 2015:- CCM Yawataka watendaji wanaohusika na suala la ugavi wa umeme Tanesco kuondoa tatizo la kukatika nishati hiyo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, October 08, 2015

KAMPENI URAIS CCM 2015:- CCM Yawataka watendaji wanaohusika na suala la ugavi wa umeme Tanesco kuondoa tatizo la kukatika nishati hiyo.

Magufulika Style  inavyozidi kushika kasi,Davis Mosha mgombea ubunge jimbo la Moshi mjini na madiwani wa Moshi mjini wakimagufulika jukwaani kuonyesha ukakamavu wao.


 Sehemu ya Umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika viwanja vya mashujaa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,jana October 07,2015, jioni kwenye mkutano wa kampeni,mkoani Kilimanjaro.

Katika mkutano wake wa Moshi mjini Dkt. Magufuli amewaonya watendaji wa Shirika la Umeme nchini TANESCO na kuwaambia kama wanazima umeme makusudi ili kuwafanya wananchi waichukie serikali wanafanya makosa na ole wao kwa vitendo hivyo visivyo vya kistaarabu, Amewaambia kwamba bado siku 17 za kampeni akichaguliwa na wananchi na kuapishwa kuwa Rais atawashughulikia ipasavyo kwani  wanajulikana.  “Katika siku hizi zilizobaki watubu wafanye kazi usiku na mchana ili umeme upatikane bila kukatika na kuleta adha kwa wananchi vinginevyo akiingia Ikulu atalala nao mbele”,alisema Dkt Magufuli huku uwaja mzima ukilipukwa kwa mayowe.

Sehemu ya Umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika viwanja vya mashujaa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,leo jioni kwenye mkutano wa kampeni,mkoani Kilimanjaro.

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika viwanja vya mashujaa Kumsikiliza alipokuwa akijinadi na kuwaga sera zake katika kuomba kura za kuwania nafasi ya Urais kwa kipindi cha awamu ya tano,kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
 
 Sehemu ya Umati wa Wananchi wa mji wa moshi waliofika katika viwanja vya mashujaa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,jana October 07,2015, jioni kwenye mkutano wa kampeni,mkoani Kilimanjaro alipokuwa akijinadi na kuomba kura za kutosha ili aibuke kuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad