KAMPENI URAIS UKAWA 2015:-Picha 6 za Edward Lowassa mbele ya Wananchi wa Babati na Mto wa Mbu Oct 02. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 03, 2015

KAMPENI URAIS UKAWA 2015:-Picha 6 za Edward Lowassa mbele ya Wananchi wa Babati na Mto wa Mbu Oct 02.

Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA Edward Lowassa October 2, 2015 alisimama mbele ya Wananchi wa Jimbo la Babati Mjini katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kwaraha, Babati Manyara.

l2
Mgombea  huyo wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa ameingia mjini Monduli na akiwa monduli kazi yake ya kwanza aliyoifanya ni kumtangaza Bw Julius Kalanga kuwa mrithi wake wa kiti cha ubunge jimbo la Monduli.

Mgombea huyo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa kipindi cha miaka 20, amewashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa ushirikiano waliompatia uliowezesha kupatiakana kwa maendeleo ndani ya jimbo hilo huku akiahidi kuendelea kutekeleza ahadi ambazo bado hajazikamilisha.

Edwrad Lowassa ametumia jukwaa la mto wa mbu wilayani Monduli kuwaomba watanzania kuhakikisha wanampigia kura nyingi zaidi kwani uwezo, nia na sababu ya kuwa mshindi wa kiti cha urais anao.
L1
l3
l4
l5
l6
Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli kwa Chadema kupitia mwamvuli wa UKAWA, Julius Karanga, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Barafu, Mto wa Mbu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni

Wakati Edward Lowassa akiwa amepita Babati mjini na Mto wa Mbu, Mama Regina Lowassa alikua Dar es salaam akizungumza na Wanawake, UNAWEZA KUMSIKILIZA HAPA CHINI…


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad