KAMENI URASI UKAWA 2015:-Lowassa aomba kura Jimbo la Ngara kwa kishindo huku Mbowe akiondoa utata nani Mgombea Ubunge. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, October 14, 2015

KAMENI URASI UKAWA 2015:-Lowassa aomba kura Jimbo la Ngara kwa kishindo huku Mbowe akiondoa utata nani Mgombea Ubunge.

Umati wa Wakazi wa mji wa Ngara,mkoani Kagera, ukiwa umefurika kwa wingi katika viwanja vya posta ya zamani kumsikiliza  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo,CHADEMA, Mh. Edward Lowassa alipopita Leo October 14,2015,kwenye Mkutano wa hadhara wa kampeni na kuwaomba Watanzania kuhakikisha wanamchagua kwa kura nyingi zaidi kwani serikali itakayoundwa chini ya umoja huo itahakikisha inarejesha katiba ya wananchi,kuboresha sekta ya elimu nchini,kutengeneza ajira kupitia JKT, sambamba na Kutatua kero za Walimu Nchini.
Katika mkutano huo wa Kampeni, Freeman Mbowe ni mwenyekiti wa Chadema taifa,alimtangaza rasmi Dr Peter Bujari kuwa mgombea Ubunge Jimbo la Ngara kupitia CHADEMA na UKAWA na hivyo kuondoa utata uliokuwepo kati ya chadema na NCCR Mageuzi,kwa kuzingatia vigezo vya makubaliano ya Viongozi wa juu wa UKAWA.

Mgombea wa urais Edward Lowassa ameendelea kupata mapokezi ya kifalme ambapo hii leo October 14,2015 amehutubia mikutano mikubwa minne katika majimbo ya Ngara mjini na Rulenge, Bilaharamuro kabla ya kuhitimisha kwa kishindo katika uwanja wa masumbwe mjini Mbogwe.

Mgombea huyo wa urais Edward Lowassa na timu yake ya kampeni anatarajiwa kuhitimisha kampeni zake kanda ya ziwa kwa kuhitimisha kwa wilaya zote zilizoko ndani ya jiji la Mwanza.




PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp  +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad