TASWIRA YA MSIBA:-Ni Nyumbani kwa Marehemu Filikunjombe. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, October 16, 2015

TASWIRA YA MSIBA:-Ni Nyumbani kwa Marehemu Filikunjombe.


Chopa iliyosababsha kifo cha Filikunjombe, Capt. William Silaa na watu wengine wawili jana Jioni, October 15,2015.


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Mapinduzi Bw Deo Filikunjombe amefariki kutokana na ajali ya Helikopta iliyotokea kwenye hifadhi ya wanyama ya Selous, pamoja na rubani Kepteni William Silaa, mfanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, wakati akitokea Dar es Salaam kwenda Ludewa.

 Wengine waliofariki kwenye ajali hiyo ni Vitalis Blanka Haule na Ofisa Tawala wa Wilaya ya Tarime, Bw. Egdi Mkwera ambaye alikuwa mtaalam wa mifugo.

Kamishna wa oparesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini Bw Paul Chagonja amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ikihusisha Helikopta yenye namba 5Y - DKK katika kijiji cha Mtende mkoani .

Kamishna Chagonja amesema polisi na taasisi nyingine ikiwemo mamlaka ya usalama wa anga wameanza uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya helikopta inayodaiwa kuwa ilikuwa imekodiwa na Bw Deo Filikunjombe.

Aliyekuwa Mbunge wa Ludewa kwa tiketi ya CCM, Deogratias Filikunjombe, enzi za uhai wake.
filikunjombe (2)

Mke wa marehemu Deogratias Filikunjombe, Sarah Filikunjombe (kushoto) akilia kwa uchungu baada ya kupata tarifa za kifo cha mumewe.
filikunjombe

Ndugu, jamaa na marafiki wakionekana wenye huzuni nyumbani kwa Deogratias Filikunjombe.
filikunjombe (3)

Nyumbani kwa Deogratias Filikunjombe Mbagala Kijichi, Dar es Salaam.
silaa

Capt. William Silaa enzi za uhai wake.
chopa

Filikunjombe akiwaaga wananchi wake.
chopa 2

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad