VPL 2015/2016:-Matokeo yote ya Ligi kuu Vodacom yapo Hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 21, 2015

VPL 2015/2016:-Matokeo yote ya Ligi kuu Vodacom yapo Hapa.

Mashabiki wa timu ya Simba ‘Mnyama’ walishindwa kuzuia furaha zao baada ya Hamisi Kiiza kuipa Simba ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa Jana September 20,2015.

Na sasa Simba SC inakwenda kambini Zanzibar kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC wikiendi hii hapo hapo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mashabiki wakishangilia ushindi wa timu yao... Simba SC imepata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Kagera Sugar.
Mashabiki wa timu ya Simba wakizawadia fedha mshambuliaji wa timu hiyo Hamisi Kiiza aliyefunga magoli matatu kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Mashabiki wa timu ya Simba wakizawadia fedha mshambuliaji wa timu hiyo Hamisi Kiiza aliyefunga magoli matatu kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar na kuwa HAT TRICK ya kwanza ya msimu huu 2015/2016 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.
Hamisi Kiiza akipokea zawadi ya fedha kutoka kwa mashabiki wa timu ya Simba

Pichani ni Hamisi Kiiza akipokea zawadi ya fedha na kofia kutoka kwa mashabiki wa timu ya Simba SC ambapo Baada ya mpira kumalizika baadhi ya mashabiki walioukuwa wamekaa karibu na lango kuu la kuingilia na kutokea uwanjani, walimwita mshambuliaji huyo aliyetupia hat-trick ya kwanza msimu huu na kumpa zawadi za pesa na vitu vingine kutokana na kufurahishwa na kiwango alichokionesha Kiiza.
Kiiza zawadi 1

Kiiza hakusita kupokea fedha hizo kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakiimba wimbo wa kumsifia Kiiza wakati akitoka uwanjani. Baada ya kuzipokea zawadi hizo Kiiza aliwashukuru mashabiki hao na kuelekea vyumbani…PICHA KWA HISANI YA SHAFFIH DAUDA.

Ligi kuu Vodacom Tanzania bara 2015/2016, iliendelea jana September 20,2015 kwa michezo mitano kupigwa kwenye viwanja vitano tofauti, ukiachana na mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Kagera Sugar uliomalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 3-1 kwenye uwanja wa Taifa matokeo mengine yalikuwa kama ifuatavyo.

Azam FC imeendeleza ushindi na kuendelea kukimbizana na Simba SC na Yanga SC baada ya kuifunga timu ya Mwadui FC kwa goli 1-0 mchezo ulichezwa kwenye uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.

Bao pekee kwenye mchezo huo limefungwa na John Bocco ‘Adebayor’

Agrey Morris alitolewa nje kwa kadi nyekundu na Mwadui kuzawadiwa penati lakini mshambuliaji wa Mwadui Rashid Mandawa alishindwa kukwamisha wavuni mkwaju huo wa penati.

Kwenye uwanja wa Manungu mjini Morogoro, Mtibwa Sugar walikuwa wenyeji wa Ndanda FC na Mtibwa imefanikiwa kushinda kwa goli 2-1 dhidi ya Ndanda FC.

Magoli ya Mtibwa yamefungwa na Salim Mbonde dakika ya kipindi cha kwanza na Said Bahanuzi akafunga goli la pili kwa upande wa Mtibwa Sugar huku goli pekee la Ndanda likifungwa na Kigi Makasi.

Mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya Toto Africans umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kutofungana kwenye mchezo uliochezwa kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga.

MATOKEO VPL 2015/2016.



Jumamosi Septemba 19,2015.

Yanga SC 4 – 1 JKT Ruvu 1

Stand United 2 – 0 African Sports

Mgambo Shooting 1 – 0 Majimaji

Tanzania Prisons 1 – 0 Mbeya City



RATIBA MECHI ZIJAZO


26.09.2015 SIMBA SC YOUNG AFRICANS NATIONAL STADIUM DAR
26.09.2015 COASTAL UNION  v MWADUI FC MKWAKWANI TANGA
26.09.2015 TANZANIA PRISONS  v MGAMBO SHOOTING SOKOINE MBEYA
26.09.2015 JKT RUVU STAND UNITED KARUME DAR
26.09.2015 MTIBWA SUGAR  v MAJIMAJI FC MANUNGU MORO
26.09.2015 KAGERA SUGAR  v TOTO AFRICANS KAITABA KAGERA
27.09.2015 AFRICAN SPORTS  v NDANDA FC MKWAKWANI TANGA
27.09.2015 AZAM FC  v MBEYA CITY AZAM COMPLEX DAR


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad