KAMPENI UKAWA 2015:-Picha wakati LOWASSA akihutubia Mjini Tabora nakusema amejipanga vyema kuzitatua kero mbali mbali zinazo wakabili wananchi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 06, 2015

KAMPENI UKAWA 2015:-Picha wakati LOWASSA akihutubia Mjini Tabora nakusema amejipanga vyema kuzitatua kero mbali mbali zinazo wakabili wananchi.

Chopa iliyompakia Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ikipiga misele juu ya uwanja wa Mkutano, leo Septemba 5, 2015, mjini Tabora na kuwa amefanya mikutano ya kampeni katika  majimbo matano ya mikoa ya Kigoma na Tabora na kuwawaomba wananchiwa maeneo hayo kuungana na watanzania wengine wanaopenda mabadiliko kumchagua rais,wabunge na madiwani wa vyama vya UKAWA ili kurahisisha kazi ya kuondoa kero zinazowakabili.

 Akizungumza katika mikutano hiyo Mh.Lowasa amesema kazi ya kukabiliana na changamoto zinazoandamana wananchi kwa muda  mrefu iko ndani ya uwezo wake na viongozi wenzake wa ukawa na itakuwa  nyepesi  zaidi kama  wananchi  watatoa  ushirikiano.

Mh.Lowassa ambaye ameweza kuwafikia wananchi wengi wa vijijini baada ya kuanza kutumia CHOPA amesema UKAWA imejipanga kikamilifu na kutumia sera zilizoko kwenye ilani ya kutatua kero nyingi zinazowakabili wananchi kinaachotakiwa  sasa ni ushirikiano wa wananchi.

 Mh.Lowassa anaendelea na kampeni katika majimbo ya mkoa wa Tabora na baadaye  Shinyanga.......Habari na :-itv.

Aliekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja akiuhutubia Umati wa wakazi wa Mji wa Tabora, waliofutirika kwa wingi kwenye Uwanja wa Town School, kulikofantika Mkutano wa Kampeni za kunadi sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, jana Septemba 05, 2015....PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.





Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wake, Mh. Freeman Mbowe, wakati wakitoka kwenye Mkutano wa hadhara wa Kampeni, Mjini Tabora,jana Septemba 5, 2015.


Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana na Mke wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa, wakati alipowasini kwenye Uwanja wa Town School, kuhudhulia Mkutano wa Kampeni, jana Septemba 5, 2015 na
wamewaomba  wananchi kuwachagua viongozi wa UKAWA wakiwemo madiwani  na waabunge  ili kutimiza lengo la mabadiliko.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, akilakiwa kwa shangwe na wananchi wa mji wa Tabora, wakati akipita kuelekea jumwaa kuu, wakati wa Mkutano wa Kampeni za kunadi sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.



 Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia wananchi wa Mji wa Tabora, hapo jana Septemba 5, 2015.



Mabadilikooooooo......" Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia na kunadi sera zake kwa wananchi wa Mji wa Tabora, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika ,jana Septemba 5, 2015.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad