Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni
wakiwa wamesimama pamoja na wananchi wa Jiji la Arusha walifurika kwa wingi
kwenye Uwanja wa Kamandolu,jana Agosti 15, 2015, wakati wa kuimba wimbo wa
Taifa.
|
Muasisi Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei akizungumza na
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho,
Mh. Edward Lowassa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kamandolu, hapo jana Agosti
15, 2015, kulikofanyika Mkutano wa kumtambulisha.
|
Pichani ni Muasisi Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei akizungumza na
maelfu ya wananchi wa Jiji la Arusha, wakati akimtambulisha Mgombea Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward
Lowassa, wakati wa Mkutano wa kutafuta udhamini wa Tume ya Uchaguzi na kutambulishwa
kwa Mgombea huyo na Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, uliofanyika kwenye Uwanja
wa Kimandolu, jana Agosti 15, 2015.
|
Mbunge wa
Jimbo la Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa
hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi wa Mgombea Urais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,pamoja na kutambulishwa kwa wananchi, uliofanyika
Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu, Jijini Arusha.
|
Pichani juu ni mgombea
mwenza Mh.Duni Hajji na pichani chini ni Mgombea Urais wa CHADEMA kupitia umoja wa UKAWA Mh.Edward Lowasana ambao
wameendelea kuwataka wananchi kudumisha
umoja na ushirikiano ili waweze kushinda
uchaguzi na kupata nafasi ya kukabiliana
na matatizo mbalimbali yanayowakabli wananchi.
|
Katika mkutano huo wa jana August
16, 2015 ,kambikuu ya upinzani katika siasa za Tanzania, imezidi kuimarika kwakumpokea
Omari Ayubu Kimbau, kada machachari wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akihamia
Chama cha Wananchi (CUF) anakotarajia kupewa dhamana ya kugombea ubunge jimboni
Mafia, Mkoa wa Pwani sambamba na Bw. Lawrance Masha.
Masha, waziri wa mambo ya ndani kwa
awamu ya kwanza ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete (Novemba 2005/2010),
alipigwa kumbo katika uchaguzi mkuu uliopita, jimbo la Nyamagana, jijini Mwanza
analowakilisha Ezekiel Wenje.
“Maamuzi magumu yamefanyika hivi leo, lakini
ni maamuzi muhimu sitaongea leo. Nitangaze tu kwamba nimejiunga rasmi Chadema,”
amewaambia wana-UKAWA waliojazana viwanja vya Tindigani. Masha ni mtoto wa Dk.
Fortunatus Masha, aliyestaafu siasa akiwa Chama cha United Democratic Party
(UDP) alikofikia ngazi ya makamu mwenyekiti.
Amehama CCM siku chache baada ya
kuthibitisha kutupwa na CCM katika uteuzi kutokana na kushindwa kura za maoni
safari hii akiomba kugombea jimbo la Sengerema.
Baada ya mkutano wa Arusha, Lowassa,
ambaye alihama CCM tarehe 28 Julai,2015 akijibu pigo la kukatwa jina katika
walioomba uteuzi wa kugombea urais, akiwa miongoni mwa waombaji 38, atakuwa
jijini Mwanza leo hii Jumapili August 16,2015.
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment