Sheria ya
mitandao Nchini Tanzania, inaanza kutumika rasmi tarehe September 01, 2015.
Zingatia haya mambo 10 muhimu ili
sheria hii isikukamate.
1. Epuka
Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari
kwa jamii yetu kupitia mitandao
2. Epuka
Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea
kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao
3. Epuka
Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia
mitandao mbalimbali ( Whatsapp, Facebook, YouTube, Instagram n.k)
4. Epuka
Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi
mbalimbali ama mitandao ya kijamii
5. Epuka
Kushiriki kusambaza chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu (kutuma kama
ulivyopokea ) itakugharimu
6. Epuka
Wizi kupitia mitandao mbalimbali na mitandao ya simu utakugharimu.
7. Epuka
Kumpatia mtu line yako ya simu na kutumika kufanyia wizi ama utapeli
itakugharimu
8. Epuka
Kushiriki kumchafua mtu,taasisi,kikundi cha watu kwa namna yoyote kupitia
mitandao pia itakugharimu.
9. Epuka
Kupoteza simu bila kutoa taarifa na kufunga mawasiliano hayo yanaweza kupelekea
kutumika kufanya uhalifu na ukaangukia hatarini
10. Epuka
Kutumia mtandao kwa utapeli kupitia 'brand' ama jina la mtu itakugharimu.
Hukumu
Ni kifungo
cha miaka kadhaa gerezani ama faini ya fedha isiyopungua milioni 5 kulingana na
kosa lililofanyika (au vyote!).
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Sunday, August 16, 2015
MUHIMU SANA:- Yafahamu Mambo 10 ya Kuepuka Ili Sheria ya Mtandao (2015) Isikupitie.....
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment