URAIS 2015 TANZANIA:-Ni Chief Lutasola Yemba mgombea urais Tanzania Bara na Said Miraji Abdullah mgombea mwenza wakipitishwa na Mkutano mkuu ADC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 06, 2015

URAIS 2015 TANZANIA:-Ni Chief Lutasola Yemba mgombea urais Tanzania Bara na Said Miraji Abdullah mgombea mwenza wakipitishwa na Mkutano mkuu ADC.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chief Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha mgombea mwenza wake, Said Miraji (kulia), katika mkutano mkuu wa tatu wa chama hicho uliofanyika Dar es Salaam August 05,2015.

 Kushoto ni mgombea urais wa chama hicho, Zanzibar, Hamad Rashid Hamad.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chief Lutasola Yemba (kulia), na mgombea mwenza wake, Said Miraji, wakiwapungia mkono wanachama wa chama hicho katika mkutano mkuu huo.



Kwa upande wake mgombea wa Tanzania Urais kwa tiketi ya chama cha ADC Bwana Chifu Lutasola Yemba , ameilalamikia serikali kwa kuingilia mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na baadhi ya taasisi kushindwa kudhibiti matumizi ya fedha katika kampeni za siasa za vyama mbalimbali hali inayoendelea kusababisha kupatikana viongozi wanaopenda mamlaka zaidi kuliko kutatua matatizo yanayowakabili watanzania.

Mgombea urais wa chama cha ADC,  Zanzibar, Hamad Rashid Hamad, akihutubia katika mkutano huo , amehasa watanzania kutambua kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu unagubikwa na gilba nyingi zikiwemo za matumizi makubwa ya fedha hali inayohatarisha mfumo wa domkrasia katika uchaguzi wa viongozi.
Mwenyekiti wa chama cha ADC  Said Miraji Abdallah akizungumza mara baada ya kutangazwa kugombea nafasi ya kuwa mgombea mweza kupitia chama hicho katika mkutano wa kamati kuu uliofanyika katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam





Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad