![]() |
|
Wasifu wa
Edward Lowassa
Hata hivyo
mchujo wa chama ulipofanyika jina lake lilikatwa mapema kabla hata ya kupelekwa
kwenye vikao vya vya juu vya chama hicho. Ambapo baadae Waziri wa Ujenzi John
Pombe Magufuli ndiye aliyeibuka kidedea na kuwa mgombea kupitia chama tawala
CCM.
Lowassa ameushutumu
mchakato CCM wa kutafuta mgombea urais akiuita kuwa ulijaa chuki na mizengwe
dhidi yake, hali ambayo aliifananisha na ‘ubakaji wa demokrasia’
“Nitakuwa
mnafki nikisema bado nina imani na CCM. CCM niliyoiona Dodoma si CCM
niliyokulia”, alisema, na kuongeza “kama Watanzania hawapati maendeleo kupitia
CCM basi wakayatafute nje ya CCM”
Wakati
sakala la Richmond lilipoibuka miaka michache tu iliyopita, Chadema ilimfanya,
limsakama Lowassa kuwa ni mmoja wa mafisadi wakubwa nchini. Lakini wakati chama
hicho kinamkaribisha kuwa mwanachama wao, kiligeuka na kusema hakuna mtu msafi
nchini na kwamba hawawezi kuacha kumpokea mwanasiasa mwenye mtaji mkubwa wa
wafuasi kama Lowassa.
Wakati akiwa
Waziri Mkuu, Lowassa alisifika kama mchapakazi hodari na msimamiaji wa moja kwa
moja wa shughuli za serikali. Bado anaendelea kufahamika kwa jina la utani la
‘mzee wa maamuzi magumu’.
Moja ya
mafanikio makubwa ya uwaziri mkuu wake ni jitihada kubwa na mafanikio ya
upatikanaji wa fedha za kujenga chuo kikuu cha Dodoma. Chuo hiki kikuu cha umma
kilichopo katikati ya Tanzania kilianzishwa mwaka 2007.
Lowassa ni
mashuhuri pia kwa kusimamia mpango wa serikali uliofanikiwa wa ujenzi wa shule
za kata ambazo uliiletea Tanzania sifa kubwa kwa kutoa fursa ya watoto wengi
kupata nafasi shuleni.
Mtoto wa
Mzee Ngoyai Lowassa, ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa serikali ya kikoloni,
Lowassa ameanza harakati zake za kuwania urais tangu mwaka 1995 lakini
inaarifiwa kwamba rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Nyerere alimkatalia
kushika nafasi hiyo. Wafuasi wa Lowassa wamekuwa wakiyatupilia mbali madai hayo
Ulipofika
uchaguzi wa mwaka 2005, Lowassa hakutaka kuwania urais, lakini badala yake
alimnadi rafiki yake wa siku nyingi Rais wa sasa Jakaya Kikwete ambaye alipata
ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 80.
Source:-BBC Swahili.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Thursday, August 06, 2015
MBIO ZA URAIS TANZANIA 2015:- Ufahamu Wasifu wa Edward Lowassa mgombea UKAWA.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.










No comments:
Post a Comment