MBIO ZA UBUNGE 2015:-Fahamu kuchugua fomu kwa Migamba ACT, Mbunge Mnyika na Adam Malima kutoridhishwa na kura za maoni CCM. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 05, 2015

MBIO ZA UBUNGE 2015:-Fahamu kuchugua fomu kwa Migamba ACT, Mbunge Mnyika na Adam Malima kutoridhishwa na kura za maoni CCM.

Mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akiangushwa kura za maoni CCM na ambaye alisema kuwa hakuridhishwa na mwenendo mzima wa kura za maoni kwa vile umechukua siku tatu bila mawakala kusaini fomu za matokeo.

NIPASHE | 5th Aug 15

Mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha,  Adam Malima amesema kuwa kura za maoni zilizopigwa jimboni humo hazikuwa huru na haki kwa madai kwamba waliopiga kura walikuwa wachache lakini kura za matokeo zikawa nyingi.

Akitangaza matokeo hayo, Mkurugenzi wa  Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Hadija Kusaga, alisema kuwa waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 46,904, kura zilizopigwa ni 26,949 na kwamba kura 904 ziliharibika.

Alisema kuwa katika matokeo ya kura hizo, mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Abdallah Ulega, aliibuka na ushindi kwa kupata kura 16, 294 huku Malima akipata kura 8, 212. Aliwataja wagombea wengine kuwa ni Shukuru Ngweshani kura 356, Jafari Ndande kura 479 na Maulid Zolange Kura 809.

NIPASHE | 5th Aug 15

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema), ameshinda katika kura za maoni za kugombea ubunge katika Jimbo la Kibamba kwa kupata kura 65  kati ya kura 80 zilizopigwa (asilimia 65).

NIPASHE | 5th Aug 15

Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba , amechukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Ubungo ambako atapambana na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Said Kubenea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

HABARI LEO | 5th Aug 15.

Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Chiku Abwao ndiye atakayepeperusha bendera ya ACT kuwania ubunge wa Jimbo la Iringa mjini katika uchaguzi mkuu ujao, huku akitamba kwamba atambwaga mbunge anayemaliza muda wake, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema).

Mbali na Abwao aliyejiunga na ACT Wazalendo hivi karibuni, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chadema, Abuu Changawa naye ameiacha Chadema na kujiunga ACT Wazalendo, huku akitangaza kuwania udiwani katika Kata ya Mivinjeni, mjini hapa.

Abwao aliyewahi kuwa mbunge wa NCCRMageuzi, alisema; “Nimeondoka Chadema baada ya kubanwa kila kona na Mchungaji Msigwa akidhani kwamba mimi nilikuwa Chadema kwa sababu ya kutaka cheo.”



Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad