Tume ya
Uchaguzi Tanzania (NEC) imewaengua wagombea urais wa vyama vya Ada-Tadea, DP, CCK na AFP jana August 21,2015 kwa maelezo kuwa wamekosa vigezo vya kugombea nafasi hiyo kubwa ya uongozi
hapa nchini.
Kwa mantiki
hiyo, Mchungaji Christopher Mtikila (DP), Godfrey Malissa (CCK) na John Chipaka
(Ada-Tadea) hawatashiriki katika kinyang’anyiro hicho baada ya fomu zao
kuonekana kuwa zina kasoro huku mgombea urais wa AFP, Omari Sombi akiungana na
wanasiasa hao kutogombea baada ya kushindwa kurejesha fomu ya urais.
Kwa mujibu
wa Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, wagombea wa vyama vinane kati ya 12
vilivyochukua fomu, wamekidhi matakwa ya sheria ya mchakato huo, hivyo
wanaruhusiwa kuanza kampeni rasmi leo August 22,2015.
Amewataja
wagombea waliopitishwa na NEC ni Dk. John Magufuli (CCM), Edward Lowassa
(Chadema), Fahmi Dovutwa (UPDP), Macmillan Lyimo (TLP) na Chief Lutalosa Yemba
(ADC).
Wengine ni
Anna Mghwira (ACT-Wazalendo) , Hashimu Rungwe (Chaumma) na Malik Kasambala
(NRA).
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp
+255789925630.
|
No comments:
Post a Comment