Polisi
wakiwa wameshika silaha za moto katika kijiji cha Maroro, Wilayani Mwanga mkoa
wa Kilimanjaro, na Msafara huo ulikuwa
na viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani ambao ni pamoja na Mbunge wa Moshi
Mjini, Phillemon Ndesamburo, Joseph Selasini (Rombo), Mbatia na na Mwenyekiti
wa TLP, Augustine Mremaambaye pia ni Mbunge wa Vunjo pamoja na viongozi wa
Chadema ngazi ya mkoa na wilaya.
|
Msafara wa
Edward Lowassa ulizuiwa kuelekea kumzika mwanasiasa mkongwe Peter Kisumo huko
Usangi.
|
Mgombea
urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa akiwa katika gari na Mheshimiwa
Philemon Ndesamburo wakati Jeshi la Polisi,
jana August 13, 2015 lilipouzuia msafara
wake wa kwenda Usangi, wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro kushiriki mazishi ya
kada wa CCM, Peter Kisumo, likitaka kupunguzwa kwa idadi ya watu.
|
Lowassa
akizungumza na baadhi ya watu waliofika baada ya msafara wake kuzuiwa na polisi
ambapo pia Mbali na kuzuia msafara huo, chombo hicho cha Dola kimepiga marufuku
shughuli za kutafuta udhamini kwa wagombea urais wa vyama vya siasa kuambatana
na misafara.
|
Lowassa,
ambaye amepitishwa na Chadema kugombea urais na ambaye ataungwa mkono na vyama
vinne vya NCCR-Mageuzi, NLD, Chadema na CUF, anatarajiwa kuanza kusaka
wadhamini leo August 14,2015 mkoani Mbeya na baadaye ataelekea Mwanza.
|
Kutokana na
kauli hiyo, Mbatia, ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) aliwataka madereva wa bodaboda kutoa bendera zao na
kutoongozana na msafara, agizo ambalo walilitii na kuondoka lakini polisi
walikataa magari kuvuka kizuizi hicho.
Baadaye,
Mbatia alizungumza kwa simu na Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu kabla ya kumpelekea simu Lowassa ambaye naye
alizungumza naye na kusema wameruhusiwa, lakini askari waliokuwa wameweka doria
walikataa kuwaruhusu.
Kutokana na
hali hiyo, Mbatia baadaye alizungumza kwa simu na kudai anawasiliana na Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Mponji lakini askari waliokuwapo walidai kuwa
wamepewa maagizo kuzuia msafara huo.
Msafara huo
ulikaa eneo hilo zaidi ya saa mbili na baadaye polisi waliruhusu gari ya Lowassa, Mbatia na Ndesamburo kupita,
lakini watu waliokuwa kwenye msafara wabaki kitendo ambacho viongozi hao
walikipinga na kuamua kurudi Moshi.
“Tumeongea
na IGP, RPC lakini tunaambiwa OCD amekataa, tunataka Watanzania wajue kuwa CCM
wameanza kupasua amani ya Taifa hili,” alisema Mbatia.
|
Msafara wa
Lowassa ulizuiwa kuelekea kwenye mazishi ya aliyekuwa waziri mkuu na mwasisi
mwenza wa CCM Peter Kisumo
|
Msafara wa
Edward Lowassa baada ya kuzuiwa kijiji cha Maroro. Picha na Chadema Blog.
|
No comments:
Post a Comment