Matokeo ya Tarime
Mjini na Tarime Vijijini ambako Nyangwine ameanguka, yamethibitishwa na Kaimu
Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu Wazazi Wilaya ya Tarime, Mathias
Lugola aliyetangaza rasmi matokeo ya majimbo hayo.
Awali, matokeo
hayo ya kura za maoni yaliahirishwa kutangazwa kutokana na kuwepo kwa tuhuma za
kuwapo kwa wizi wa kura. Kwa jimbo la Tarime Mjini, Lugola alifafanua kuwa
Michael Kembaki ndiye aliyeibuka mshindi kwa kura 3,908 akifuatiwa na Kabaka
aliyepata kura 2,411.
Katika Jimbo la
Tarime Vijijini, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Christopher Kangoye ambaye amejaribu
zaidi ya mara tatu kuusaka ubunge, lakini bila mafanikio aliibuka mshindi
akivuna kura 15,928 dhidi ya 12,205 za John Gimunta ambaye ni Mweka Hazina wa
CCM wilayani Tarime.
Nyangwine na
Gimunta, baadaye walilalamikia matokeo hayo wakisema mchakato wa kura za maoni
ulitawaliwa na hujuma.
Kayombo azidiwa
Mbinga Katika Jimbo la Mbinga Vijijini, matokeo yaliyotangazwa saa 5:45 usiku
baada ya mvutano wa kutangaza matokeo unaodaiwa kudumu kwa takribani saa 12,
yameonesha kuwa mbunge wa jimbo hilo aliyekuwa amejitokeza kutetea kiti chake,
Gaudence Kayombo ameshindwa katika kura za maoni ndani ya CCM.
Aliyeibuka mshindi
ni Martin Msuha, aliyepata kura 13,354 dhidi ya 12,068 za Kayombo, ambaye pia
kwa mwaka mmoja na nusu kati ya Januari 12, 2007 na Agosti 2, 2008 alikuwa
Naibu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji.
Wengine
walioshiriki katika mchakato wa ubunge jimboni humo na kura zao kwenye mabano
ni Humphrey Kisika (545), Dk Silverius Komba (1,289), Edesius Kinunda (2,355),
Deodatus Mapunda (2,532), Benaya Kapinga (3,941) na Deodatus Ndunguru.
Wabunge Singida
hoi , MCHUANO wa makada mbalimbali wa CCM kuwania nafasi za ubunge katika mkoa wa
Singida umekamilika, huku wabunge waliokuwa wakitetea nafasi zao na baadhi ya
vigogo kwenye chama hicho wakiwa wamebwaga vibaya.
Kwa mujibu wa
Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Singida, Mary Maziku, wabunge
wawili waliokuwa wakitetea nafasi zao hawakuweza kupata kura za kutosha kwenye
kura za maoni. Nao ni Salome Mwambu wa Jimbo la Mkalama na John Lwanji wa
Manyoni Magharibi.
Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Singida, Mgana Msindai ambaye aligombea jimbo la Mkalama alifanikiwa
kushika nafasi ya pili kwenye kinyang’anyiro hicho kwa kupata kura 3,908 nyuma
ya Allan Kiula aliyezoa kura 5,823. Jimbo hilo lilikuwa na wagombea 16.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Wednesday, August 05, 2015
STORI KUBWA:-Ni kuhusu Mawaziri waliokatwa kura za Maoni CCM.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment