MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2015:-Tazama Taswira Picha ulivyokabidhiwa Mkoani Kagera ukitokea Kigoma na miradi iliyotembelewa na Mbio hizo kwa mwaka huu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 05, 2015

MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2015:-Tazama Taswira Picha ulivyokabidhiwa Mkoani Kagera ukitokea Kigoma na miradi iliyotembelewa na Mbio hizo kwa mwaka huu.

Mwenge wa Uhuru ukiwa eneo la Kalenge wilayani Biharamulo mkoani Kagera tayari kukabidhiwa mkoani Kagera Agosti 02,2015 kuanza mbio zake mkoani humo ukitokea Mkoani Kigoma ambapo Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali msaafu Issa Machibya (mwenye suti nyeusi) ameema Mwenge huo ukiwa Kigoma ulizindua, kukagua na kuweka mawe ya msingi miradi 52 yenye thamani ya Sh.19.87 bilioni.


Mkuu wa mkoa wa Kigoma ,Kanal mstaafu Issa Machibya ( kushoto ) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa mkoa wa Kagera,Bw.John Mongela ( kulia ) eneo la Kalenge wilayani Biharamulo mkoani Kagera ili kuanza mbio zake ambapo ukiwa mkoani Kagera, Jumla ya miradi 52 ya maendeleo ya wananchi yenye thamani ya Sh 13.88 bilioni, iilizinduliwa,kufunguliwa na kuwekewa mawe ya msingi mkoani Kagera,katika wilaya saba kabla ya mwenge huo wa uhuru kukabidhiwa mkoawa Geita Agosti 10 mwaka huu 2015.

Bw.Mongela amesema miradi hiyo imechangiwa na wadau wamaendeleo ambapo serikali kuu imechangia Sh3.35 bilioni, halmashauri za wilaya Sh 2 bilioni, wananchi Sh5.4 bilioni kwa lengo la kuchochea maendeleo ya kijamii,katika sekta ya elimu, maji, kilimo, Afya, uvuvi, hifadhi ya mazingira,vikundi vya ujasiriamali pamoja na Vikundi vinavyojihusisha na mikopo kwa wananwake na vijana.





Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka huu 2015,Bw.Juma Khatib Chum akisalimiana na baadhi ya Viongozi mara baada ya kufungua Maktaba ya shule ya sekondari Nyantakara wilayani Biharamulo mkoani Kagera ambapo Jumla ya shilingi milioni 141 zimetumika kujenga maktaba  hiyo ya shule  chini ya ufadhili wa mgodi wa dhahabu wa TULAWAKA kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya hiyo.





Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad