Goli kipa Ally
Mustafa ‘Barthez’ amepangua penalti mbili na kuiwezesha Yanga SC kutwaa Ngao ya Jamii 2015/2016 baada ya kuifunga
Azam FC kwa penalti 8 -7 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 jioni ya leo August
22, 2015 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam...Picha kwa hisani ya BIN ZUBEIRY.
Barthez
alipangua penalti za beki raia wa Ivory Coast, Serge Wawa Pascal na mshambuliaji Ame Ali ‘Zungu’, wakati kipa wa Azam FC, Aishi Manula naye alicheza
penalti ya Nahodha wa Yanga SC, Nadir
Haroub Ali ‘Cannavaro’ ikapanguliwa.
Penalti za
Yanga SC zilifungwa na Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Amissi
Tambwe, Andrey Coutinho, Godfrey Mwashiuya, Thabani Kamusoko, Mbuyu Twite na
Kelvin Yondan aliyepiga ya mwisho.
Penalti za
Azam FC zilifungwa na Kipre Herman Tchetche, Nahodha John Raphael
Bocco, Himid Mao Mkami, Aggrey Morris, Jean Baptiste Mugiraneza, Erasto Nyoni
na Shomary Kapombe.
|
Yanga SC
wakifurahia Ngao yao baada ya kuifunga
Azam FC Septemba 14, mwaka Jana 2014.
Bao pekee la
Salum Telela mwaka 2013 liliipa Yanga SC ushindi wa Ngao, wakati mwaka jana
2014, mabao mawili ya Mbrazil Genilson Santana Santos ‘Jaja’ na moja la Simon
Msuva yaliipa tena timu hiyo taji hilo.
Yanga SC
hadi sasa ndiyo timu iliyotwaa mara nyingi zaidi Ngao ya Jamii, kuanzia mwaka
2001 ikiifunga 2 -1 Simba SC na 2010 ikiwafunga tena watani wao hao kwa
penalti 3 -1 baada ya sare ya 0-0 ndani
ya dakika ya 90 na mwaka juzi 2013 na mwaka jana 2014 ikiifunga Azam FC.
Inafuatia
Simba SC iliyotwaa Ngao mara mbili, 2011 wakiifunga Yanga SC 2 - 0 na 2012
wakiifunga Azam FC 3-2, wakati Mtibwa Sugar ni timu nyingine iliyowahi kutwaa
Ngao mwaka 2009 ikiifunga 1-0 Yanga SC.
MABINGWA WA
NGAO YA JAMII.
2001: Yanga
SC 2-1 Simba SC
2009: Mtibwa
Sugar 1-0 Yanga SC
2010: Yanga
SC 0-0 Simba SC (3-1 penalti)
2011: Simba
SC 2-0 Yanga SC
2012: Simba
SC 3-2 Azam FC
2013: Yanga
SC 1-0 Azam FC
2014: Yanga
SC 3-0 Azam FC
LIGI KUU VODACOM 2015 / 2016 –
RATIBA.
Jumamosi Septemba 12,2015.
Ndanda v
Mgambo Shooting (Nang’wanda - Mtwara)
African
Sports v Simba SC (Mkwakwani - Tanga)
Majimaji v
JKT Ruvu (Majimaji - Songea)
Azam FC v
Tanzania (Azam Complex – Dar es Salaam)
Stand United
v Mtibwa Sugar (Kambarage - Shinyanga)
Toto
Africans v Mwadui (CCM Kirumba - Mwanza)
Jumapili Septemba 13,2015.
Yanga v
Coastal Union (Taifa – Dar es Salaam).
Kocha wa
Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm akimpongeza kipa Ally Mustafa 'Barthez'
baada ya mechi jioni ya leo August 22, 2015 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Picha kwa hisani ya BIN ZUBEIRY.
|
No comments:
Post a Comment