MKUTANO MKUU CHADEMA 2015:-Lowassa, Duni rasmi urais UKAWA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, August 04, 2015

MKUTANO MKUU CHADEMA 2015:-Lowassa, Duni rasmi urais UKAWA.

Mgombe urais @EdwardLowassa (Kushoto) Makamu wa Rais Haji Duni na Mgombe urais Zanzibar Mh Maalim Seif #Mkutano Mkuu CHADEMA 2015-Dar es Salaam leo Agosti 04,2015.

MKUTANO Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa pamoja wamempitisha kwa kishindo Bw.Edward Lowassa ,aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania kuwa mgombea urais kupitia Chadema na Umoja wa Katiba Ukawa ambaye atapambana na wagombea wengine akiwemo Dr.John Pombe Magufuli kutoka CCM kwenye uchaguzi mkuu hapo Octoba 25,mwaka huu..

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es Salaam leo Agosti 04,2015 na pia umempitisha Mgombea mwenza Bw.Juma Duni Haji katika kura zilizopigwa kwa kanda kuulizwa na Mwenyekiti wa Taifa Chadema ,Freeman Mbowe.
NUKUU MKUTANO MKUU CHADEMA 2015:-Pamoja tuwe mashahid wa historia,nchi yetu ina ndoto ya mabadiliko,ili ndoto ikamilike tunahitaj kila mtu aliye tayari

@EdwardLowassa akipongezwa na Mh Freeman MBowe baada ya Kupitishwa kuwa mgombea urais kupitia Chadema na #UKAWA
# MKUTANO MKUU, Mbowe amsajili Mgana Msindai Mwkt Mkoa wa Singida CCM kujiunga na Chadema .
#MKUTANO MKUU 2015-Bw. Mbowe amsajili Munge wa Arumeri Magharibi Mh. Ole Medeye kujiunga na Chadema.
#MKUTANO MKUU Mbowe amsajili Mh. Makongoro Mahanga Naibi waziri ajira na kazi mbunge wa segere CCM kujiunga Chadema .
#MKUTANOMKUU 2015 -M/kiti wa NCCR Mageuzi Mhe. James Mbati akimpongeza Mhe. @EdwardLowassa .
NUKUU MKUTANO MKUU CHADEMA 2015:-Pamoja tuwe mashahid wa historia,nchi yetu ina ndoto ya mabadiliko,ili ndoto ikamilike tunahitaj kila mtu aliye tayar i



Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad