|
Baada ya
kuwasili katika ofisi hizo, wagombea hao walitumia muda wa dakika 27
kukamilisha zoezi la kuchukua fomu kisha kurejea katika viwanja vya ofisi za
CCM makao makuu Lumumba kuungana na Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa
CCM aliyeongozana na mkewe Salma Kikwete, kuhutubia mamia ya wanachama wa chama
hicho waliojitokeza kuwasindikiza wagombea kuchukua fomu.
Akizungumza
baada ya kukaribishwa na Kinana, Rais Kikwete alinzakuzungumza huku akivirushia
dongo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwamba wamechukua
“makapi ya CCM” huku akisema, “ Wale wanaodhani CCM ni ya mchezo watakiona cha
mtema kuni.
Huku
akiongeza kuwa watu wenye tama kupitiliza Tumejiandaa vya kutosha na
tutashinda. Uwezo tunao, maarifa tunayo tutashinda. Tujipange kwa hoja za
kuzungumzia uzuri wa CCM.”
“CCM
jiandaeni kushangilia ushindi….Utawala bora upo, demokrasia ipo, uhuru wa
habari upo, watu wanajiunga na vyama vya siasa kwa uhuru, uchumi unakuwa na
maendeleo yanaendelea kupatikana,” amesema Rais Kikwete.
|
No comments:
Post a Comment