MCHUJO UEFA:-Matokeo ya klabu 5 kati ya 10 kufanikiwa kufuzu Hatua ya Makundi ya UEFA Champions League 2015/2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 26, 2015

MCHUJO UEFA:-Matokeo ya klabu 5 kati ya 10 kufanikiwa kufuzu Hatua ya Makundi ya UEFA Champions League 2015/2016.

RAUNDI YA MWISHO YA MCHUJO UEFA 2015/2016.

Marudiano-Matokeo/Jumanne Agosti 25,2015.

Dinamo Zagreb 4 – 1 Skenderbeu  [6-2]

Malmo 2 – 0 Celtic  [4-3]

Maccabi Tel Aviv 1 – 1 FC Basel  [3-3, Maccabi yasonga]

AS Monaco 2 – 1 Valencia  [3-4]

Shakhtar Donetsk 2 – 2 Rapid Vienna  [3-2] 

Matokeo hayo yanazifanya klabu  5 kati ya 10  kufanikiwa kufuzu Hatua ya Makundi ya UEFA Champions League 2015/2016 baada ya kukamilisha Mechi zao za Marudiano hapo jana August 25,2015 usiku na zikiacha Klabu nyingine 5 zitakazojulikana baada ya Mechi zao za leo Jumatano August 26,2015 Usiku.

Celtic ya Scotland, iliyoshinda Mechi ya kwanza 3-2 kwao, Leo imetupwa nje na sasa itacheza EUROPA League, baada ya kuchapwa 2-0 na Malmo ya Sweden.

Nao AS Monaco, licha ya kuifunga Valencia 2-1, wametupwa nje baada kufungwa 3-1 katika Mechi ya kwanza huko Spain.
Klabu nyingine zilizofuzu hii kucheza Makundi ni Dinamo Zagreb ya Croatia, Maccabi Tel Aviv ya Israel iliyopita kwa Bao za Ugenini baada Mechi zao zote mbili kuisha Sare za 2-2 na 1-1, na Shakhtar Dobetsk ya Ukraine.

Timu hizi 5 zilizofuzu zitaungana na nyingine 5 zitakazopatikana Leo Usiku na kutumbukizwa kwenye Droo ya Makundi pamoja na Timu nyingine 22 ambazo zitaanzia Makundi.

Droo hii ya Makundi itanyika Ijumaa August 28,2015 huko Monaco ili kupanga Makundi 8 ya Timu 4 kila moja.

UEFA CHAMPIONZ LEAGUE - RAUNDI YA MWISHO YA MCHUJO.

Marudiano - Saa 3 Dakika 45 Usiku.

Jumatano Agosti 26,2015.

APOEL Nicosia v Astana [0-1]

Partizan Belgrade v BATE Borisov [0-1]

Bayer Leverkusen v Lazio [0-1]

CSKA Moscowv Sporting CP [1-2]

Club Brugge v Manchester United [1-3]

PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad