![]() |
|
Uzinduzi wa
kampeni za UKAWA Kitaifa katika viwanja vya Jangwani Jumamosi hii tarehe
29.8.2015, Hapo jana August 25, 2015, Mgombea Urais wa tiketi ya UKAWA, Edward Lowassa pamoja na mgombea mwenza, Juma Duni walitembelea
sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam kujionea na kuzungumza na watanzania
wa kipato cha chini ili kuyaelewa matatizo yao.
Pia walisafiri
kwa daladala kufahamu kwa ukaribu changamoto zao za usafiri.
Jumamosi wiki
hii Katika uzinduzi wa kampeni ,Wagombea hao wanatarajiwa kueleza suluhisho ya
changamoto hizo pamoja na sababu kwanini wananchi wanahitaji kuchagua
mabadiliko ifikapo Oktoba 25,2015, Tuko tayari kusimamia na kuongoza
mabadiliko.
|






![]() |







No comments:
Post a Comment