UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2015/2016:- Matokeo ya Mechi jana August 26, 2015 na Makundi yatakavyopangwa leo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 27, 2015

UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2015/2016:- Matokeo ya Mechi jana August 26, 2015 na Makundi yatakavyopangwa leo.

Hapo jana August 26, 2015, Katika muendelezo wa mechi za mkondo wa pili kufuzu kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya, timu kadhaa zilishuka dimbani kutafuta tiketi ya kuingia katika hatua ya makundi.

Manchester United imefanikiwa kusonga mbele kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Club Brugge na kufanya matokeo kuwa 7-1, katika mikondo yote miwili.

Katika mchezo huo nahodha Wayne Rooney alidhihirisha kuwa bado yupo vizuri katika kucheka na nyavu, baada kufunga mara tatu.

APOEL Nicosia 1 – 1 Astana  [1-2]

Partizan Belgrade 2- 1  BATE Borisov  [2-2, BATE yasonga kwa Goli la Ugenini]

Bayer Leverkusen 3 – 0 Lazio  [3-1]

CSKA Moscow 3 – 1 Sporting CP  [4-3]

Club Brugge 0  - 4 Manchester United  [1-7]

Droo ya makundi ya ligi hiyo, inatarajiwa kufanyika leo hii August 27,2015 ambapo Kila Chungu kitakuwa na Jumla ya Timu 8 ambapo kila Chungu kitatoa Timu 1 kuunda Kundi moja la Timu 4 lakini Klabu toka Nchi moja hazitawekwa katika Kundi moja.

Hivyo, Mabingwa Watetezi FC Barcelona, Chelsea, Bayern München, Juventus, Benfica, Paris Saint-Germain, Zenit and PSV Eindhoven zote zipo Chungu Namba 1 na hivyo haziwezi kupambanishwa.

Pia safari hii Bingwa wa EUROPA LEAGUE 2014/2015, ambae ni Sevilla, ameingizwa moja kwa moja kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE na hii imeifanya Spain iwe Nchi ya kwanza kabisa kuwa na Timu 5 kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE ukizijumuisha Barcelona, Real Madrid, Atletico Madrid na Valencia iliyofuzu kutoka Mechi za Mchujo.

TIMU ZIPI ZIPO KWENYE CHUNGU KIPI.

***Kila Chungu kina Jumla ya Timu 8 mbapo kila Chungu kitatoa Timu 1 kuunda Kundi moja la Timu 4 isipokuwa Timu za Nchi moja hazitawekwa Kundi moja. 

CHUNGU NAMBA 1: Barcelona, Chelsea, Bayern München, Juventus, Benfica, Saint-Germain, Zenit St Petersburg, PSV Eindhoven.

CHUNGU 2: Real Madrid, Atlético Madrid, FC Porto, Arsenal, Valencia, Manchester City, Manchester United, Bayer Leverkusen

CHUNGU 3: Olympique Lyonnais, Dynamo Kyiv, Olympiacos, Galatasaray, Roma, Shakhtar Donetsk, Sevilla, CSKA Moscow

CHUNGU 4: Borussia Mönchengladbach, Wolfsburg, Dinamo Zagreb, Maccabi Tel-Aviv, Gent, Malmo, Astana, BATE Borisov

TAREHE MUHIMU:

-Droo Hatua ya Makundi: Agosti 27,2015.

-Ratiba Mechi za Makundi: 

Mechidei 1: 15/16 Septemba

Mechidei 2: 29/30 Septemba 

Mechidei 3: 20/21 Oktoba

Mechidei 4: 3/4 Novemba 

Mechidei 5: 24/25 Novemba 

Mechidei 6: 8/9 Decemba

Raundi za Mtoano:

-Droo ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16: Desemba 14,2015

**Mechi Februari 16/17/23/24 na Marudiano Machi 8/9/15/16

-Droo ya Robo Fainali: Machi 18,2016

**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13

-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15,2016

**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4

FAINALI

Mei 28,2016.

San Siro, Milan, Italy

PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad