KUTOKA CUF/VIDEO AUGUST 06,2015:- Profesa Lipumba katangaza maamuzi Magumu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 06, 2015

KUTOKA CUF/VIDEO AUGUST 06,2015:- Profesa Lipumba katangaza maamuzi Magumu.

Leo Al hamisi ya August 06, 2015  ambapo Mwenyekiti wa C.U.F Prof. Ibrahim Lipumba kakutana na Waandishi wa habari Dar es salaam kutangaza maamuzi yake magumu siku chache baada ya Edward Lowassa kujiunga na UKAWA.

Tamko hilo la Prof. Lipumba linahitimisha siku mbili za minong’ono na tetesi zilizogubika medani ya kisiasa nchini kuwa kiongozi huyo anaondoka katika chama hicho hali iliyolazimu wananchama, wapenzi na mashabiki wa kiongozi huyo kufurika makao makuu ya chama hicho Buguruni Dar es Salaam jana ili kujua hatma ya kiongozi wao huyo.

Akizungumzia sababu za kujiuzulu kwake, Profesa Lipumba amesema amekerwa na hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao CUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.

Amesema Ukawa ulianzishwa kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa wanaipinga Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wa nchi kupitia umoja huo.

Prof. Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.

SIKILIZA /TAZAMA VIDEO YA MKUTANO WAKE HAPA CHINI.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad